Emmanuel Simwanza katika moja ya mechi zake akiwa na Mwadui FC |
BEKI mpya wa Simba, Emmanuel Semwanza, amesema Simba ni chama lake tangu enzi akiwa anasoma shule ya Msingi.
Simba ilimsainisha mkataba wa miaka miwili beki wenye uwezo wa kucheza kati juzi usiku akitokea Mwadui FC baada ya kumaliza mkataba .
Ujio wa beki huyo katika kikosi cha timu hiyo kutaleta ushindani mkubwa wa namba kutokana na kuwepo wa Novaty Lufunga pamoja na Jjuuko Murushid ambao wote wanachezana beki ya kati.
Semwanza amesema kwamba amesaini kuitumikia timu hiyo sio kwa kuangalia maslahi kama ilivyokuwa inafikiriwa na baadhi ya wadau wa soka.
Alisema ametimiza ndoto zake za kuichezea timu aipendayo hivyo atahakikisha anaonyesha ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake kuhakikisha wanafanya vizuri.
“Suala la nini nitaifanyia Simba kwa sasa ni mapema, nafurahi kwanza kuchezea timu ambayo ilikuwa ndoto yangu tangu nikiwa shule, nitahakikisha najituma kwa kucheza kwa mapenzi na sio maslahi,” alisema.
Semwanza alisema anaimani kutokana na mapenzi yake aliyokuwa nayo katika timu hiyo hatokubali kuona wanapoteza hivyo atajituma kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kuhakikisha anaendana na wenzake.
“Kusugua benchi kwa mara ya kwanza sio ajabu, hivyo baada ya kuonyesha kiwango changu kazi ya kunitumia itakuwa jukumu la kiongozi wa benchi la ufundi ambaye ni kocha,” alisema.
0 comments:
Post a Comment