Monday, June 13, 2016

Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia wamechezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Peru na kutupwa nje ya michuano ya Copa America katika hatua ya makundi kwa mara kwanza baada ya miaka 30.

Brazil ilikuwa haijapoteza mchezo dhidi ya Peru katika kipindi cha miaka 16 iliyopita na walikuwa wakihitaji pointi moja pekee kufuzu kwenye hatua ya robo fainali.

Raul Ruidiaz aliyeingia kutokea benchi aliifungia Peru bao pekee na la ushindi dakika ya 75 kwenye uwanja wa Foxborough Stadium huku bao hilo likilalamikiwa na Brazil kuwa mpira uligosa mkono wa mfungaji kabla ya kutinga wavuni.

Ecuador wakaichapa Haiti kwa bao 4-0 na kufuzu hatua ya nane bora kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo tangu mwaka 1997.

Brazil wameshindwa kupata ushindi mbele ya Peru na Ecuador, ushindi wao kwenye hatua ya makundi ulikuwa ni dhidi ya Haiti waliowachapa bao 7-1.

Baada ya game, kocha wa Brazil aliulizwa swali na waandishi wa habari kama anahofia kibarua chake kuota nyasi, akajibu; “Nahofia kifo pekee, siogopi kusuhu hicho unachokisema.”

“Ukifanya kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Brazil unatakiwa kuwa tayari kukosolewa timu isipopata matokeo, lakini kiundani tunajua tunachokifanya.”

Dunga amelalamikia goli lililofungwa na Ruidiaz ambaye alitumia mkono kuunganisha krosi ya Andy Polo.

Wachezaji wa Brazil walimvaa refa wa mchezo huo mruguay Andres Cunha wakipinga goli hilo lakini baada ya mawasiliano na fourth official alisimamia uamuzi wake wa awali kutoa goli hilo kwa Peru.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video