Saturday, June 11, 2016

March 10 mwaka 2012 ndiyo mara ya kwanza kwa ndugu wawili  Taulant na Granit Xhaka kukutana wakiwa katika vilabu tofauti. Wakati huo Granit akiichezea FC Basel na kutinga uzi namba 13 na Taulant akiichezea Grasshopper na kutinga jezi namba 34. Katika mcheo huo Basel waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Katika kipindi hicho ilikuwa ni vigumu kutabairi ambacho kinatokea leo kingekuja kutokea yaani wawili hawa kupambana tena wakiwa katika mataifa tofauti.

Wawili hao, sio tu walikuwa ndugu bali marafiki wakubwa. walikulia katika academy ya Basel, lakini Taulant ambaye alikuwa na mkubwa kwa miezi 18 zaidi Granit alikuwa kwa mkopo. Asili ya baba yao ilikuwa ni  Abania. Mwaka 1989, alihamia Uswizi kutokana na hali ya machafuko huko Albania na hapo ndipo tofauti ilipotokea.

Tofauti hiyo ndio imezua gumzo kwenye michuano hiyo ya Euro. Leo Granit na Taulant wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne, lakini safari hii ikiwa ni katika mazingira tofauti kabisa. Granit atakuwa akiiwakilisha Uswizi  ambayo alijidhihirisha nayo tangu mwaka 2011wakati Taulant atakuwa akiiwalikisha Albania ambayo alianza kuichezea mwaka 2014. Umeona picha lilivyokuwa tamu sasa, yaani ndugu wawili waliozaliwa na baba na mama mmoja wanachezea mataifa tofauti.

Hii inanikumbusha wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 wakati ndugu wengine wawili walipokutana wakati wakicheza katika mataifa mawili tofauti. Hawa ni Kevin-Prince Boateng na Jerome Boateng. Kevin akichezea Ghana na Jerome Ujerumani. Ghana walikutana na Ujerumani robo fainali na Ghana kutupwa nje. Lakini wawili hawa (Granit na Taulant) wanaingia katika historia mpya Ulaya.

Wazazi wao Ragip na Elmaze, walikuwa ni miongoni mwa maelfu ya watu walioingia Uswizi wakitokea Albania katika eneo la Kosovo wakati huo ikiwa bado ni sehemu ya iliyokuwa Yugoslavia kutokana na vita kali iliyokuwa ikiendelea. Waliwazaa watoto wao wakati huo wakiwa katika mji wa Basel. Wachezaji wengine wa Uswizi wenye asili ya Albania ni Shaqiri na kiungo wa Watford Valon Behrami.

Albania ndiyo chanzo kikubwa cha Granit kuchezea Uswizi. Hapo awali Granit alionesha dhamira yake ya dhati ya kuchezea taifa la Albania, lakini Shirikisho la soka nchini humo lilionesha kutokuwa tayari na huduma yake na ndipo alipoamua kuchukua maamuzi ya kuchezea Uswizi. Kwa upande wake Taulant aliamua kuvuta subira ili kuichezea Albania. Na ndipo milango ilipofunguka baada ya kuitwa katika mchezo wa kundi I dhidi ya Ureno na Albania kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

"Familia ni kitu muhimu sana kwangu", Granit alisema katika mahaojiano yaliyofanyika miaka mitatu iliyopita.
"Hasa kaka yangu Taulant....tunaongea mambo mengi sana".

Tangi enzi na enzi Granit na Taulant wamekuwa na ukaribu mkuwa na walilelewa katika kituo kimoja cha kukuzia vipaji cha Concordia Basel ambapo wazazi wao waliwapeleka ili kuacha kuzurura mitaani wakati huo wakiwa na umri wa miaka minne na sita mtawalia. Utofauti wao wa uraia kamwe haujawatengenisha. Mara kadhaa Granit amekuwa akipost vitu kweny mitandao ya kijamii kuonesha support yake kwa Albania na Kosovo ambao nao wamekuwa ni wanachama wa FIFA na UEFA.

Hali hiyo ilianza kuleta sintofahamu kidogo lakini hata hivyo kwa sasa Granit amesema mawazo yake yote yako kwa Uswizi na anachoangalia kwa sasa ni mchezo wao dhidi ya Albania utakaopigwa katika uwanja wa Stade Bollaert-Delelis

Punde tu baada ya droo kufanyika, tuliingiwa na hali ya kutoamini kuhusu suala hili, lakini kwa sasa tumeshazoea na kuichukulia hali kama ilivyo na naamini mchezo utakuwa mzuri", Granit alisema mapema wiki hii.

Macho ya mashabiki na wadau wengi wa soka yakuwa si tu kuangalia Albania na Uswizi, bali Granit na Taulant wakifanya shughuli pevu katikati ya dimba, 'battle' ya wenyewe kwa wenyewe.
Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa Stade Bollaert-Delelis majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video