Tuesday, May 17, 2016

Wachezaji watano wanaweza wasiwe na uhakika wa kubaki katika kikosi cha Yanga wakati kikijiandaa na msimu ujao.

Yanga imeanza kujiimarisha mapema kwa ajili ya msimu ujao ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo. Tayari imeshamnasa Hassan Kessy kutoka Simba kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na Juma Mahadh ambaye ametokea Coastal Union. 

Kessy amesajiliwa kwa dau la shilingi milioni 40 na Mahadh amepewa Sh mil 30. Lakini wakati hao wakiingia, wengine watano wanatoka.

Chanzo kimeeleza nyota hao watano huenda wataachwa waende nje ya kikosi au kutolewa mkopo kutokana na kutokutoa mchango mkubwa msimu huu. 

Chanzo hicho kiliwataja wachezaji hao kuwa ni Paul Nonga ambaye yeye mwenyewe aliomba kuondoka kutokana na kushindwa kuonyesha ushindani mbele ya Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Wengine ni Mniger, Issoufoe Boubacar, Salum Telela huku kipa Benedicto Tinoco na kiungo mkabaji, Said Juma Makapu wakitolewa kwa mkopo kutokana na kocha kutokubali uwezo wao.

“Benchi letu la ufundi tayari limepokea ripoti ya usajili kutoka kwa kocha wetu wakati ligi kuu ikielekea ukingoni na kikubwa amepanga kukiboresha kikosi chake ili kilete ushindani.

“Hivyo basi, katika ripoti hiyo kocha ametoa mapendekezo ya kuwaacha baadhi ya wachezaji huku wengine tukiwatoa kwa mkopo kwa ajili ya baadhi ya wachezaji kupata nafasi ya kuviendeleza vipaji vyao.

“Kati ya wachezaji hao watano, liliondolewa jina la kiungo wetu Twite (Mbuyu) ambaye alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji tutakaowaacha, lakini baadaye tukaamua kumuacha kwa ajili ya michuano ya kimataifa kutokana na uzoefu alionao,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro kuzungumzia hilo, alisema: “Hilo suala linamhusu kocha ambaye anahusika na masuala ya ufundi, hivyo ni vema akatafutwe yeye kwa ajili ya kufafanua kila kitu.

“Halafu isitoshe hiki siyo kipindi cha kutangaza wachezaji wa kuwaacha, hivyo ni vema mkatupa muda zaidi, sasa hivi wachezaji na benchi la ufundi lipo kwenye shamrashamra ya ubingwa wa ligi.”
Chanzo:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video