Sunday, May 22, 2016

England wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uturuki, kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Etihad jijini Manchester, mchezo maalum wakujipima nguvu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya EURO 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi June.
Magoli ya England yamefungwa na Harry Kane katika dakika ya 3 na Jamie Vardy dakika ya 83 huku goli pekee la Uturuki likifungwa na  Hakan Calhanoglu baada ya kuunganisha krosi murua ya Volkan Sen.
Hata hivyo England walikosa penati iliyopigwa na Harry Kane baada ya Vardy kufanyiwa madhambi na kipa wa Uturuki dakika ya 72.

Takwimu muhimu za mchezo.

  • Jamie Vardy sasa amefunga katika mechi tatu mfululizo akiwa na timu yake ya taifa ya England.
  • Harry Kane amekuwa mchezaji wa kwanza wa England kukosa penati (za ndani ya dakika 90) tangu mara ya mwisho alipokosa Frank Lampard dhidi ya Japan May 2010.
  • England wamefunga penati 11 zilizopita kabla ya Kane kukosa leo.
  • Hakan Calhanoglu amefunga la kwanza kwa taifa lake dhidi ya England baada ya kukutana takriban mara 11.
  • England wamecheza michezo mitatu yote wakiruhusu mabao, ikiwa ni mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo kwa mara nne mfululizo August 2013.
  • Roy Hodgson ni kocha wa 6 wa England kufikisha michezo 50 games (wengine wakiwa ni Walter Winterbottom, Alf Ramsey, Ron Greenwood, Bobby Robson na Sven-Goran Eriksson).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video