Thursday, May 26, 2016

Kuelekea fainali ya UEFA May 28 siku ya Real Madrid watakuwa wakijaribu kutwaa taji la 11 katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati, Atletico watakuwa wakijaribu kulitwaa kwa mara ya kwanza mara baada ya kulikosa mara mbili wakifika hatua ya fainali.
Mbali ya kuwa katika jiji moja na kupambana kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid na Atletico Madrid wanatofautiana kwa vitu vingi sana.
Real Madrid ni klabu yenye fedha nyingi na yenye nguvu kubwa ambapo pia imejaza mastaa wenye majina makubwa ulimwenguni. Atletico kwa upande wao, ni klabu ambayo inapambana kutokana na nguvu zao wenyewe na kutafuta mafanikio kwa kutumia wachezaji ambao kamwe hawana majina makubwa ulimwenguni, wengi wao wakiwa hawajulikani.
Vilabu hivi viwili vinacheza staili mbili tofauti, vile vile wana 'fan base' mbili zenye nguvu tofauti.
Mtazamo wao tofauti kwenye mchezo wa Jumamosi utakaopigwa jijini Milan kwenye dimba la San Siro, ndiyo utakaoleta ladha nyingine tena nzuri kutokana n ushindani utakaokuwepo, ambapo bila ya kusahau ni miaka miwili tu imepita tangu wanaume hao wawili wakutane katika fainali ya michuano hii, na Real kushinda kwa kishindo katika muda wa ziada kwa magoli 4-1. Ndani ya dakika tisini walifungana bao 1-1.
“Mara zote katika hatua kama hii, uzoefu umekuwa ni kitu muhimu sana, na katika nyanja hiyo sisi tuna faida kubwa kidogo zaidi ya wenzetu”,Cristiano Ronaldo alisema katika moja ya mahojiano yake na waandishi. “Atletico watakuwa makini sana kutokana na kile kilichowatokea miaka miwili iliyopita tulipowafunga katika fainali. Watakuwa wakihitaji ushindi kwa namna yoyote na sisi tuko tayari kupambana.”

Tuchungulie kwa karibu utofauti uliopo kati ya klabu hizi mbili:

HISTORIA
Wakati Real Madrid ni mabingwa mara nyingi zaidi kwenye ligi ya La Liga na UEFA, Atletico ndiyo kwanza wanaanza kupambana kuwa washindani halisi licha ya kutokuwa na kiwango cha fedha walau kinachokaribiana na Real ambao kwa sasa ndio wanaongoza kwa utajiri duniani.
Hii ni mara ya 14 kwa Real Madrid kuingia fainali huku wakilisaka taji lao la 11, wakati Atletico watakuwa wakilisaka taji lao la kwanza baada ya kulikosa katika fainali mbili ambazo ni mwaka 1974 dhidi Bayern Munich na 2014 dhidi ya Real.
“Huu ni mchezo muhimu sana kwetu, kwa faida ya klabu na mashabiki wetu”, Diego Godin ambaye ni beki wa Atletico alisema. “Tunafarijika sana kwa jinsi timu yetu inavyofanya kutokana na njia tuliyopitia. Tuna fursa nyingine ya kuhakikisha tunachukua taji hili safari hii.”
Safu ya ushambuliaji hatari ya Real Madrid ianyoongozwa Ronaldo, itakuwa na wakati mgumu pale itakapokuwa ikipana na ukuta mgumu wa Atletico ya Diego Simeone.
Real Madrid ni moja ya timu zenye safu hatari ya ushambuliaji ambayo imeweka kambani mabao 27, mabao matatu pungufu dhidi ya Bayern Munich. Atletico wamefunga mabao 16 ambayo ndiyo idadi ya mabao Ronaldo anayo mpaka sasa.
“Tunataka kupata ushindi mnono siku ya Jumamosi, ambao ndio utatoa muelekeo wa timu yetu,” Ronaldo amesema. “Tunaamini kuwa tutafanikiwa juu ya hilo.”

Wachezaji
Wakiwa na nguvu kubwa ya pesa ya kusajili mchezaji yeyote ulimwenguni, Real Madrid ina wachezaji ghali kama Ronaldo, Karim Benzema, Gareth Bale, Sergio Ramos and Marcelo. Atletico, ambayo pengine pato lake ni nusu tu ya pato la mahasimu wao, watakuwa wakiwategemea washambulizi wao kama vile Fernando Torres na Antoine Griezmann, bila ya kusahau mabeki wao mkongwe Diego Godin na Filipe Luis.

Makocha
Zinedine Zidane, kiungo matata ambaye alishinda kombe la UEFA akiwa na Real Madrid mwaka 2002, anakuwa katika kibarua chake cha kwanza kama kocha wa Madrid kuiongoza Madrid kufika fainali baada ya kuchukua mikoba kwa mtangulizi wake Rafa Benitez. Diego Simeone, kiungo mkabaji wa zamani wa Argentina na Atletico, alikabidhiwa mikoaba ya kuiona klabu hiyo mwaka 2012. Tangu hapo amekuwa ni mtu muhimu baada ya kuigeuza Atletico kuwa klabu ya watu wapambanaji, kitu ambacho ndiyo kipaumbele cha timu hiyo.
“Nina bahati kubwa ya kuwa hapa na kuishi vizuri na wachezaji pamoja na mashabiki,” Zidane amesema.
“Staili yetu ni kucheza na kuhakikisha kila mchezaji anajitolea mpaka kiwango chake cha mwisho,” Simeone amesema. “Kwangu mimi wachezaji ni watu muhimu sana wa kuamua matokea katika mchezo huo.”

Mashabiki
Real Madrid wana 'fan base' kubwa sana kuliko Atletico, na wanajulikana sana kwa kipaumbele chao cha kusaka mataji kuliko kitu chochote katika soka. Kwa upande mashabiki wa wa Atletico maarufu kama ‘colchoneros’ wao huwa wanasapoti timu yao bila kujali matokeo yakoje lakini mashabiki wa Real maarufu kama “Madridistas” ni watu wanatoa sapoti kubwa wakati timu ikiwa inafanya vizuri tu, lakini inapotokea timu haifanyi vizuri basi uwanja unawaka moto.

KUELEKEA FAINALI YAO.
Zote kwa Real Madrid na Atletico wamefika hatua hii baada ya kumaliza kileleni kwenye makundi yao. Atletico walifanikiwa kuwang'oa PSV Eindhoven kwa mikwaju ya penati katika hatua ya bora, wakawang'oa Barcelona kwa wastani wa mabao 3-2 vile vile Bayern Munich kwa goli la ugenini. Real Madrid waliwatoa AS Roma kwa wastani wa mabao 4-0, baadaye Wolfsburg kwa wastani wa mabao 3-2 na kumalizia kwa Manchester City baada ya kuwafunga na kuwatoa nje kwa wastani wa bao 1-0 katika hatua ya nusu fainali.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video