Ubingwa usiotarajiwa wa Leicester City unaweza kuwa umewafanya wawe maarufu zaidi duniani lakini Arsenal ndio timu iliyopata fedha nyingi zaidi msimu huu kwenye EPL.
Takwimu rasmi zilizochapishwa leo Jumanne zinaonyesha Gunners wameingiza kiasi cha £101million – kutoka kwenye mapato ya Premier League.
Manchester City wameshika nafasi ya pili katika listi waliopata hela nyingi – wakiingiza £96,971,603, wakifuatiwa na Manchester United (£96.5m) na Tottenham (£95.2m), huku mabingwa Leicester wakishika nafasi ya tano kwa kuingiza £93.2m. Timu iliyoingiza fedha chache zaidi ni Aston Villa, walioingiza £66.6m, fedha nyingi zaidi kuwahi kupokea timu iliyoshika nafasi ya mwisho kwenye ligi.
Fedha hizi kwa asilimia kubwa zinatoka kwenye dili kubwa la haki ya matangazo ya TV lakini pia kutoka kwenye mapato ya jumla ya kibiashara kwa kila klabu.

Kila klabu baada ya hapo inapokea kiasi cha
£1,242,405 kulingana na kila nafasi waliyoshika kwenye ligi – kuanzia chini kwa Aston Villa mpaka mabingwa Leicester waliopata kiasi cha £24,848,100.
Kila klabu pia hupata kiasi cha fedha kwa kutegemea mara ngapi wameonyeshwa mechi zao live katika Sky au BT. Kila klabu inapata kiasi cha wastani wa chini wa £8,782,088 kutoka katika mgawanyo huu, hata kama wakionyeshwa mara chache kama Watford na Bournemouth ambao mechi 8 kila timu ilipata kuonyeshwa live – Norwich City na Stoke City (mara 9 kila timu).

Arsenal walionyeshwa live UK zaidi, mara 27, wakifuatiwa na Manchester United 26 halafu City 25, Liverpool 23, na Chelsea 22.
Kwa msimu wa 2015-16 kila klabu ilipata mgawo sawa wa £55,849,800 kutokana na mapato ya kuonyeshwa mechi zao nyumbani, mapato ya nje na mapato ya kibiashara.


0 comments:
Post a Comment