Monday, May 23, 2016

Hapana shaka yoyote kwamba Jose Mourinho ndiye kocha mtarajiwa wa Manchester United licha kutotangazwa.
Hali hiyo inatokana na tetesi nyingi zinazoripotiwa huku zikichagiwa na kutimuliwa kwa alyekuwa kocha wa klabu hiyo Mdachi Louis van Gaal.
Van Gaal alikuwa ni kama mtu ambaye alikuwa amaeshakufa kwa miezi kadhaa nyuma, lakini mazishi ndiyo yamefanyika leo kutokana na kupewa taarifa ya kufukuzwa rasmi.
Sasa baada ya zoezi kuwa limekamilika, Mourinho ambaye ndiye mrithi mtarajiwa anakabiliwa na mambo kadhaa ya kufanya klabuni hapo ili kurudisha imani ya mashabiki iliyopotea kwa kipindi kirefu sasa.

Haya ndio mambo saba ambayo Mourinho anapaswa kufanya United:

1. Kurudisha ari ya ushindi kwa wachezaji kuanzia 'dressing room' mpaka uwanjani.
 
Kipaumbele cha kwanza ni lazima kuhakikisha kuwa umoja unarudi kwa wchezaji, kitu ambacho kilionekana kukosekana katika siku za usoni katika utawala wa Van Gaal.
Mourinho mara zote ni mtu mwenye misimamo na asiyeyumbishwa na wachezaji. Kama atafanikiwa kuleta ari iliyokosekana tangu kipindi cha Sir Alex Ferguson, basi United itakuwa haishikiki msimu ujao.

2. Kuondoa wachezaji wasio na hadhi ya kuchezea Manchester United.Marcos Rojo ni miongoni mwa wachezaji walio kwenye hatari ya kupitiwa na panga katika dirisha hili la usajili.

Ndani ya United kuna mchanganyiko wa wachezaji wenye hadhi na wasio na hadhi tena ya kuichezea timu hiyo – Mathalan David De Gea, Chris Smalling, Wayne Rooney , Anthony Martial – hawa wana hadi sawa kabisa na klabu.

Juan Mata huyu ana hadhi lakini tatizo kubwa maelewano yake na Mourinho si mazuri hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka, Bastian Schweinsteiger, Marcos Rojo, Morgan Schneiderlin, Phil Jones, Marouane Fellaini na Memphis Depay ni wazi kuwa watakutana na panga kabla ya dirisha kufungwa.

3. Kuleta wachezaji wenye ubora wa wazoefu.
 I
Inasemekana kuwa Mourinho ametengewa kiasi cha paundi milioni 200 kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu.
Akimleta Zlatan Ibrahimovic atakuwa ni msaada japo kwa kipindi kifupi huku akitafuta mpango wa muda mrefu, pia eneo la safu ya ulinzi linahitaji maboresho makubwa hasa kama atawapata John Stones na Marquinhos kutwakuwa na nafuu– Pai kiungo aina ya James Rodriguez atakuwa ni msaada mkubwa kwa Mourinho.

4.Kujaribu kuendana na sera ya klabu
Hapa ndipo shughuli nzito ilipo. Mourinho na United wanatofautiana hapa. Hii ni klabu ambayo imejengwa kwa misingi ya kucheza soka la kushambulia na pia falsafa ya kuwapa nafasi vijana; katika hili Mourinho si muumini sana, mara nyingi ameuwa si mtu wa kuwaamini vijana. Chini ya Van Gaal tumeona akiwapa nafasi vijana kama Rashford, Cameron Borthwick-Jackson, Jesse Lingard na wengineo, lakini Mourinho si mtu wa hivyo hasa ukifuatilia historia katika vilabu vyote alivyopita. Sasa ili kuweza kuendana na United, hili suala pia ni muhimu akalitupia jicho la aina yake ili kudumisha utamuduni wa United.

5. Matumizi bora ya uwepo wa Wayne Rooney ambaye no moja ya wachezaji aliowahi kuwahitaji.
Mourinho ni mfuasi mkubwa sana wa Rooney, alijaribu kusajili wakati akiwa Chelsea. Hakuna shaka kwamba nahodha huyo wa United amejihakikishia nafasi ya kubaki klabuni hapo huku akiwa mtu muhimu.
Lakin vipi kuhusu nafasia takayokuwa akimchezesha? Rooneya maekuwa akichezeshwa kwenye nafasi ya kiungo  tangu alipotoka kuwa majeruhi, lakini hata hivyo bado Mourinho anaamini kwamba Rooney ni mtu sahihi kukaa mbele kwenye safu ya ushambuliaji, hivyo atampa nafasi.

6. Kurudisha imani ya timu kwa mashabiki
Mashabiki wa  Manchester United wamepoteza imani na timu yao
Licha ya kuwa timu ilikuwa inafanya vibaya mwanzani mashabiki wa United walijitahidi kuonesha imani kwa kocha wa lakini kadri siku zilivyozidi kusonga mbele mambo yaliwawi vigumu na kukata tamaa. Enzi za Sir Alex Ferguson ulikuwa unahesabu umeifunga United mpaka mpira unapokuwa umemalizika, lakini siku hizi United ndio wanaomba mpira umalizike hata kama wako mbele. Hili ni jukumu la Mourinho kuifanya United irudi katika zama za Ferguson.

7. Matokeo ndio yanatakiwa kuzungumza.
Ikumbukwe tu wakati Mourinho amarudi Chelsea mwaka 2013, akiwaahidi msimu wa kwanza wamvumilie aijenge timu ili kuanza kuchukua mataji ambayo waliyamisi kwa muda mrefu. Na kweli alifanya hivyo kwenye msimu wake wa pili tu pale alipochukua ndoo ya EPL na Capital One.
Mara amekuwa ni mtu mwenye uchu wa mafanikio, akifanya hivyo basi atakuwa amejitengenezea heshima kubwa hata kama kuna matatizo mengine ya nje ya uwanja yatakuwa yakitokea.Muhimu ni yeye kufanya matokeo ya uwanjani yazungumze yenyewe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video