Sunday, May 29, 2016

Ujerumani imepokea kipigo cha tatu ndani ya mechi nne walizocheza huku jana wakiambuliwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Slovakia katika mchezo wa mwisho wa kirafiki kabla ya michuano ya Euro 2016 kuanza rasmi.
Ujerumani ambao ni mabingwa wa dunia walianza kupata bao lao dakika ya 13 kupitia kwa Mario Gomez ambaye alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati.
Lakini Slovakia, ambao wapo kwenye kundi moja na  England na Wales walitulia na kurudisha na kuongeza mabao yao kupitia kwa Marek Hamsik, Michal Duris na Juraj Kucka.
Mchezo huo ulichezwa katika mazingira magumu kutokana na mvua kubwa kunyesha hali iliyosababisha uwanja kujaa maji.
Germany, ambao wako kwenye kundi moja na Ireland ya Kaskazini wanatakiwa kukamilisha kikosi chao cha wachezaji  23 usiku wa Jumanne.
Kwingineko, mabingwa wa Euro mwaka 2012 timu ya Hispania wameendelea na maandalizi yao kwa kucheza dhidi ya Bosnia-Herzegovina na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, mchezo uliochezwa nchini Uswizi.
Mshambuliaji wa Celta Vigo Nolito ndiyo alifungua ukurasa wa mabao kwa Hispania kwa kufunga mabao mawili kabla nyota wa Chelsea Pedro kufunga la tatu.
Goli pekee la Bosnia lilifungwa na Emir Spahic.
Beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin kwa mara ya kwanza jana alivaa uzi wa Hispania.

Video

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video