Tuesday, May 24, 2016

Fernando Torres amesema kwamba kunyanyua ubingwa UEFA akiwa na Atletico yatakuwa ni mafanikio makubwa sana katika maisha yake ya soka.
Straika huyo wa Uhispania aliweza kunyakua kombe la dunia mwaka 2010 na makombe ya Ulaya mwaka 2008 na 2012, vile vile kuisaidia Chelsea kubeba ndoo ya UEFA mwaka 2012.
Lakini licha ya mafanaikio yote hayo makubwa katika maisha yake ya soka, Torres amesema kwamba hakuna kitakachozidi furaha yake endapo atafanikiwa kubeba ndoo ya UEFA na Atletico Madrid watakaovaana na Real Madrid mwishoni mwa wiki hii.
"Kama kuna kitu kinakachonipa furaha ya kipekee masihani basi ni pale nitakapotwaa kombe la UEFA nikiwa na Atletico," alisema Torres. "Nilishinda hili kombe nikiwa na Chelsea, lakini sikuwa katika nafasi nzuri wakati ule. Sikuhisi kama nilitapa huduma niliyostahili pale klabuni kwa wakati ule — sikujisikia vizuri kwa kweli.
"Nisingependa sana kuzungumzia nyakati hizo. Maisha yangu yanaenda mujarabu kwa sasa hapa Atletico, najisikia niko nyumbani, najiamini na sitaki kurudisha nyuma fikra za kipindi cha nyuma."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video