Friday, May 27, 2016

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), jana Mei 26, 2016 limetangza kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika klabu ya Yanga ya Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi tarehe 25 Juni mwaka huu.
Nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanane wa Kamati ya Utendaji.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh. 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh. 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 31 Mei, 2016.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video