Daily Mail linaripoti kuwa, kipa hodari wa Manchester United David De Gea yupo tayari kuondoka klabuni hapo katika msimu huu wa usajili wa majira ya joto, endapo tu kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal ataendelea kubaki klabuni hapo.
Mlinda lango huyo namba moja wa Mashetani Wekundu hao na Hispania, amekuwa hana furaha chini ya kocha huyo licha kusaini mkataba wa miaka minne mwanzoni mwa msimu huu.
Vyanzo mbalimbali kutoka klabuni hapo vinaeleza kwamba, De Gea, ambaye anawindwa kwa udi na uvumba na Real Madrid atahakikisha anafanya kila mbinu ili kuondoka klabuni hapo msimu huu.
Inaarifiwa kuwa, Real Madrdi wanaanda ada ya paundi milioni 40 ili kuvunja mkataba wa De Gea kabla ya kufika June 15.
Taarifa za kina kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa sababu kubwa ya Mhispania huyo kutaka kuondoka ni kile kinasemekana klabu kukosa morali hali iliyopelekea kushindwa kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
0 comments:
Post a Comment