Uhasimu katika ya vigogo wawili wa jiji la Manchester yaani Manchester United na Manchester City leo unaweza kunoga zaidi kutokana na wawili hao kuwania kwa udi na uvumba nafasi ya kushiriki UEFA mwakani.
Manchester City wana matumaini makubwa zaidi ya kuchukua nafasi hiyo endapo tu watafanikiwa kushinda mchezo wao dhidi ya wabishi Swansea City, mchezo utakaopigwa kunako dimba la Liberty (Liberty Stadium). Manchester United, ambao kwa sasa wako katika nafasi ya tano huku wakiwa pointi mbili nyuma ya Manchester City wanaomba majirani zao wapoteze huku wao wakishinda ili kuweza kupata nafasi hiyo.
Swansea inawezekana ikawa klabu ya pili kuzifunga Chelsea, Liverpool, Manchester United na Manchester City (endapo wataifunga) katika uwanja wao wa nyumbani kwenye msimu mmoja, baada ya Blackburn kufanya hivyo mwaka 1993-94.
Haya ni mambo manne ambayo unapaswa kufahamu kuelekea mchezo huo:
4. Majeruhi na taarifa nyingine muhimu kutoka kila timu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Teamtalk Swansea watapumzisha nyota wao karibu wote ambao watakuwa wakiwakilisha nchi zao kwenye michuano ya Euro mwaka 2016 katika mchezo wao wa leo ambao ndio wa mwisho kwenye dhidi ya Manchester City.
Nahodha wa Wales Ashley Williams na mwenzake Neil Taylor, Miceland Gylfi Sigurdsson na kipa Mpoland Lukasz Fabianski wote hawatajumuishwa kwenye kikosi katika mchezo huo.
Hii inaashirikia kwamba kipa raia wa Sweden Kristoffer Nordfeldt atacheza kwa mara yake ya kwanza kabisa kwenye Ligi ya England.
Swansea pia watamkosa winga wao mahiri Jefferson Montero na Alberto Paloschi ambao wanasumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja.
Kwa upande wao Manchester City, hawatakuwa na nahodha wao Vincent Kompany ambaye anasumbuliwa na maumivu ya paja, vile vile David Silva anayesumbuliwa na maumivu misuli ya paja na Pablo Zabaleta anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Lakini, beki wa kushoto Mserbia Aleksandar Kolarov anatazamiwa kuwa fiti baada ya kuthibitishwa na madkatari wa timu baada ya kuwa amekosa mchezo dhidi ya Arsenal uliopisha kwa sare ya 2-2 kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.
Samir Nasri tayari amerudi baada ya kupona malaria.
3. Matakeo ya michezo saba ya hivi karibuni
Swansea City:
Swansea City 1 – 0 Aston Villa
Stoke City 2 – 2 Swansea City
Swansea City 1 – 0 Chelsea
Newcastle 3 – 0 Swansea City
Leicester City 4 – 0 Swansea City
Swansea City 3 – 1 Liverpool
West Ham 1 – 4 Swansea City
Manchester City:
Bournemouth 0 – 4 Manchester City
Manchester City 2 – 1 West Brom
Chelsea 0 – 3 Manchester City
Newcastle 1 – 1 Manchester City
Manchester City 4 – 0 Stoke City
Southampton 4 – 2 Manchester City
Manchester City 2 – 2 Arsenal
2. Matokeo ya head-to-head – michezo mitatu ya mwisho
22 Novemba 2014: Manchester City 2 – 1 Swansea City
Yaya Toure ndiyo alikuwa shujaa kwa kuifungia City goli la pili baada ya kutoka nyuma kwa bao 1 katika dimba la Etihad.
Wilfried Bony ndiye aliifungia Swansea goli la pekee na la kuongoza, japikuwa halikutosha kuwa ushindi.
17 May 2015: Swansea City 2 – 4 Manchester City
Wilfried Bony alifunga goli lake la nne akirudi Liberty Stadium kama mchezaji wa City baada ya kuondoka Swansea.
12 Desemba 2015: Manchester City 2 – 1 Swansea City
Wakicheza kwa mara ya kwanza bila ya kocha wao Garry Monk ambaye alifukuzwa, Swansea walipiga mpira mwingi mno na ambao bado haukuzaa matunda.
Hata hivyo, kwa mara nyingine tena mshambuliaji wao wa zamani Wilfried Bony alikuwa wa kwanza kushindilia msumari wa moto baada ya dakika ya 26 ya mchezo.
1. Wachezaji muhimu
Manchester City:
Sergio Aguero: Mchezaji huyo raia wa Argentina amekuwa katika kiwango cha hali ya juu kwa takriban misimu yote. Akiwa amefunga magoli 24 kwenye ligi na kuwa nyuma kwa goli moja dhidi ya kinara Harry Kane wa Tottenham, Aguero atakuwa ndiyo hatari kubwa kwa Swansea City.
Aguero (27) atakuwa akiwania kuongeza idadi ya mabao yake ili kutetea kiatu chake.
Andre Ayew: Mghana huyo amethibitisha kwamba anaweza kufunga dhidi ya timu yoyote ile. Ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi ya England, nyote huyo wa zamani wa Marseille amefunga magoli 11, na kutengeneza nafasi za magoli 23 na kutoa pasi za magoli mbili kwa timu yake msimu huu.
Ayew (26) amezifunga baadhi ya timu kubwa msimu huu kama vile Manchester United, Chelsea, Liverpool and Tottenham. Hivyo basi, kiwango chake kinaweza kuthibitisha ni hatari kubwa kwa Manchester City leo.
0 comments:
Post a Comment