Friday, May 27, 2016

SIMBA imeamua kukata ngebe za Yanga ambayo kila kukicha imekuwa ikiwafanyia uhuni kwa kuwanyakua wachezaji wake ambao bado inawahitaji baada ya kuanza mapema harakati za kuhakikisha Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ haondoki kwenye klabu hiyo kirahisi.

BINGWA linafahamu kuwa Yanga inammezea mate Tshabalala hii ikiwa ni baada ya kumng’oa Msimbazi, Hassan Ramadhan ‘Kessy’ ambaye mkataba wake ulikuwa umemalizika, lakini ili kuhakikisha Tshabalala anabaki Msimbazi vigogo wa Simba harakati za kufanya mambo yanayoonyesha wazi kuwa wamepania kumbakiza beki huyo wa kushoto kwenye timu yao kwa muda mrefu ujao.

Harakati hizo zimeanza kufanywa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope ambaye anajipanga kumpa Tshabalala gari kutokana na nidhamu ya hali ya juu ambayo staa huyo amekuwa akiionyesha tangu atue Msimbazi.

Tshabalala aliyesajiliwa na klabu hiyo misimu miwili iliyopita akitokea Kagera Sugar, ameonyesha kiwango kilichomfanya aaminiwe na kila kocha aliyeifundisha klabu hiyo katika muda wote alioitumikia Simba.

Akizungumza na BINGWA jijini jana, Hanspope alisema ni kweli alitoa ahadi ya gari kwa mchezaji huyo Novemba mwaka jana kutokana na nidhamu aliyonayo ndani na nje ya uwanja.

Alisema katika kikosi cha Wanamsimbazi hao pia kuna wachezaji ambao wameonyesha nidhamu lakini ameshawishika zaidi na Tshabalala na atafanya kama alivyomuahidi.

“Ni kweli hilo suala lipo, ahadi niliitoa mwaka jana kutokana na jinsi alivyoonyesha kiwango kizuri pamoja na nidhamu yake, ndiyo maana nimeamua kumzawadia gari,” alisema.

Alisema ni mapema kutaja aina ya gari atakalompa beki huyo, hivyo mipango hiyo itakapokamilika jambo hilo litakuwa wazi.

Uamuzi huo wa Poppe kumpa Tshabalala gari unatafsiri kama harakati za kuhakikisha staa huyo anakuwa na furaha ndani ya klabu hiyo ili pindi atakapotakiwa kuongeza mkataba mpya awe radhi kufanya hivyo kwa sababu kwa sasa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Wakati viongozi wa Simba wakijiandaa kumpa Tshabalala gari, beki huyo amefunguka na kusema kuwa anafurahi kuona mchango wake katika timu unathaminiwa na kila mmoja hivyo anaamini juhudi zake binafsi zimemfikisha katika hali hiyo hadi kuahidiwa zawadi hiyo.

“Hilo jambo kwangu ni jipya, ila nitafurahi kusikia hivyo pia nina imani kwamba mchango wangu unathaminika katika klabu iwe viongozi, mashabiki na wanachama,” alisema.

Tshabalala alisema licha ya ahadi hiyo pia anawashuruku mashabiki kwa kumpa zawadi ya viatu aina ya Nike Mercurial kama ambavyo huvaliwa na staa wa soka wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kuahidi kuendelea kujituma na kujitolea kupambana kurejesha heshima ya Simba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video