Huenda mashabiki wa Real Madrid wakaamua kufanya maombi na dua kwa ajili ya Cristiano Ronaldo ambaye alishindwa kumaliza mazoezi pamoja na timu yake leo asubuhi kutokana na majeraha.
Akiwa leo ndiyo amerejea kwenye mazoezi ya pamoja na kikosi cha kwanza, hakuna uhakika kama Ronaldo ataweza kucheza fainali ya Champions League siku ya Jumapili dhidi ya mahasimu wao wa jiji moja Atletico Madrid.
Star huyo wa timu ya taifa ya Ureno mwenye miaka 31 inaripotiwa alisukumwa kwa nyuma na Dani Carvajal kulikosababisha kugongana na golikipa wa akiba Kiko Casilla.
Alipatiwa matibabu na daktari wa timu huku akiwa uwanjani, lakini Ronaldo hakuweza kuendelea na mazoezi na kukaa nje hadi mwisho zikiwa zimesalia siku chache kabla ya fainali ya Champions League itakayopigwa jijini Milan, Italia.
0 comments:
Post a Comment