Saturday, May 28, 2016

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid Ronaldo amemsifu Diego Simeone na kusema kuwa ni kocha mzuri, lakini akikiri kwamba hajawahi kuwa mpenzi wa mbinu za kocha huyo.
Simeone anakutana na mahasimu wake Real Madrid katika fainali itakayopigwa leo San Siro jijini Milan, akisaka kulipa kisasi baada ya kupoteza fainali ya mwaka 2014.
"Kiukweli  huwa navutiwa sana na aina ya mpira vizuri na wa kuvutia," Ronaldo aliliambia La Gazzetta dello Sport.
"Simeone ana viashiria vya hasira za Kiargentinian na sasa anavihamishia kwa wachezaji wake. Vitu ambavyo binafsi sivipendi, lakini ukiachana na hayo, Simeone ni kocha mzuri.
"Wachezaji wake hucheza vizuri sana, wanashambulia na wanakaba, pia ni wagumu kufungika. Wana mtindo wa kipekee na ni vigumu sana kuendana nao".
Ronaldo ameshawahi kucheza Real Madrid na kwa nyakati tofauti aliwahi kukutana na Simeone akiwa Atletico, vile vile walishawahi kucheza pamoja kunako klabu ya Inter Milan.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video