Monday, May 30, 2016

Kushinda taji la Champions League ni jambo kubwa sana kwa kocha yoyote barani Ulaya, ni jambo linaleta heshima kubwa na kujenga historia miongoni mwa makocha bora Ulaya. Lakini kwa Real Madrid linaweza kuwa jambo lenye utofauti kutokana na asili ya uendeshaji wa klabu hiyo.
Unaweza kuwapa ndoo ya UEFA lakini endapo msimu ujao unashindwa kuwapa taji, basi kibarua kinaota nyasi kama ilivyotokea kwa Ancelotti.
Licha ya kuwapa Real Madrid  kombe la UEFA kwa mara ya 11 (Undecima), Zinedine Zidane ana kazi kubwa ya kufanya ili kuendelea kudumu klabuni hapo ikiwemo kuendelea kuwa na mahusiano bora na Ronaldo.
Zidane mara zote amekuwa si mtu wa kuendekeza malumbano na wachezaji na hicho ndicho kinachompa heshima kubwa klabuni hapo ukiachana na histoaria yake klabuni hapo. 
Zidane aliichukua Madrid kutoka kwa Benitez wakati ikiwa katika hali mbaya na hata kutopewa nafasi ya kufanya vyema La Liga na Champions League kwa ujumla.
Lakini kwa kipindi kisichopungua miezi mitano tangu achukue timu hiyo kutoka kwa Benitez, Zidane amewapa ndoo ya UEFA pamoja na kushika nafasi ya pili pungufu ya pointi moja tu nyuma ya mabingwa Barcelona.
Hii inaashiria nini?, inaashiria kwamba, maamuzi ya rais Florentino Perez kumtimua Benitez mwezi January na kumkabidhi mikoba Zidane yalikuwa ni sahihi. 
Perez alikosolewa vikali baada ya kumfukuza Benitez katikati ya msimu, lakini ukweli ni kwamba kosa lake kubwa lilikuwa ni kumfukuza Ancelotti wakati wa msimu wa majira ya joto kutokana na kushindwa kuipa Real kombe lolote, basi badala ya kumpa timu Benitez, wangempa Zidane kutokana na historia yake na klabu hiyo.
Zidane alikuwa kocha msaidizi wa Ancelotti wakati Madrid wakibeba La Decima mwka 2013-14 na vilevile ana historia ya kufunga goli muhimu mwaka 2002 dhidi ya Bayer Liverkusen na na kuipa Real ndoo ya nane ya UEFA wakati huo. Ana heshima kubwa kwa wachezaji kutokana na historia ya aliyonayo klabuni hapo ukiachana na hisia zake juu ya klabu hiyo.
Licha ya ukweli kwamba njia ya Madrid UEFA mpaka kufika fainali haikuwa ngumu kiasi hicho na hata ushindi wao katika fainali dhidi ya Atletico umekuja kwa njia ya matuta, lakini si kila kocha angeweza kufanya hivyo ilhali Zidane amefanikiwa kufanya hivyo.
Zidane amekitumia kikamilifu kikosi hicho hicho ambacho Benitez alikuwa  akikitumia, isipokuwa Danilo na James Rodriguez, ambao Zidane amekuwa hawatumia badala yake akiwatumia Dani Carvajal na Casemiro.
Uwepo wa Casemiro katika nafasi ya kiungo na  Dani Carvajal kama beki wa kulia umekuwa ukitoa balansi kubwa kwa timu ukilinganisha na wakati ule wa Benitez alipokuwa akimchezesha Danilo. 
Hata hivyo ukweli unabaki wazi kuwa licha ya kushinda La Undecima, Madrid wamekosa mpango madhubuti na staili ya uchezaji inayoitambulisha timu.
Kuelekea katika mapumziko kabla ya kuanza kwa msimu mpya, Zidane anapaswa kusajili wachezaji ambao anahisi wataendana na mfumo wake bila ya kusahau kuingiza rasmi falsafa zake ambazo zitatoa mwanga mpya kwa timu hiyo kuwa na mtindo maalum ambao umekosekana klabuni hapo katika miaka ya hivi karibuni.
Ikumbukwe kwamba wapinzani wakubwa wa Real La Liga ambao ni Atletico na Barcelona, wana falsafa ambazo zinatambulisha timu zao, kwa mafano Barcelona wanasifika kwa soka la kasi na pasi nyingi, huku Atletico wakisifika kwa soka la nguvu na kasi.
Katika mikakati yake ya msimu ujao lazima ahakikishe kuwa Ronaldo anaingia moja kwa moja kwenye mfumo wake. Sababu kubwa ya kusema hivyo ni kwamba Ronaldo amekuwa ni mtu muhimu katika timu hiyo, amefunga penati muhimu iliyoipa timu hiyo ndoo ya La Undecima, vile vile ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye klabu hiyo kwa sasa, kwa hiyo kwa kufanya hivyo, atakuwa amepiga hatua moja mbele.
Na kitu kizuri zaidi ni kwamba, Ronaldo mwenyewe ameahidi kuendelea kubaki klabuni hapo na ameonesha nia na shauku ya kuendelea kuichezea kuichezea Madrid hata katika siku za baadaye kama ambavyo rais wa klabu hiyo Florentino Perez alivyosema kwamba anaamini Ronald atastaafia Real Madrid. Hivyo kazi inabaki kwa Zidane mwenye kama atapata fursa ya kuendelea kubaki kuwa kocha wa Madrid misimu kadhaa mbele.
Zidane mwenyewe pia anaonekana kuwa na mahusiano mazuri na Ronaldo, na nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu alishawahi kusema kuwa, kama ataendelea kuwa kocha wa Real,basi anaamini kuwa Ronaldo pia ataendelea kubaki klabuni hapo.
Kwa kumalizia tu ni kwamba Zidane anaweza kuwa na historia kubwa zaidi ya mafanikio klabu hapo endapo tu atakuja na aina yake ya mfumo wa uchezaji utakaoitambulisha Real kama ilivyo kwa Barca na Atletico na kubwa zaidi na kutunza uhusiano wake bora na Ronaldo ili aweze kujitoa kwa ajili ya timu, kitu ambacho kitampa mafanikio na heshima kubwa sana klabuni hapo. 
Ndoo hii ya La Undecima ni mwanzo tu wa mafanikio ya Real chini ya Zidane.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video