Tuesday, May 31, 2016

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew amemwacha nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus kwenye kikosi cha wachezaji 23 kitakacholiwakilisha taifa hilo kwenye michuano ya EURO mwaka huu itakayofanyika nchini Ufaransa.
Reus alikosa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 kutokana na majeraha.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Leow amesema:

 "Yamekuwa ni maamuzi yaliyotuuma sisi na yeye [Reus], na yenye fedheha kwetu sisi.
"Marco Reus ambaye yuko fiti kwa asilimia mia moja angekuwa ni hazina kubwa sana kwetu.

"Nawashukuru sana wachezaji hawa wanne, walijitahidi sana mazoezini, walitolea kwa nguvu zao zote na ni matumaini yangu kwamba hawatofedheheshwa na jambo hili.
Haya hayakuwa maamuzi dhidi ya wachezaji wanne bali yamekuwa ni maaamuzi kwa ajili ya wachezaji 23".
Ikumbukwe tu leo ilikuwa ni birthday ya Reus na rafiki yake Mari Gotze alitweet kwenye twitter yake akisema: “Hongereza @Marco kwa siku yako ya kuzaliwa, nasubiri kwa hamu kuwa pamoja nawe katika michuano ijayo ya EURO”. 
Sasa baada ya kuona jina la rafiki yake kipenzi halipo kwenye timu ya taifa ghafla ya akaifuta tweet hiyo na kuandika "Hongera kwa siku ya kuzaliwa @Marcihno11 lakini tuna huzuni kubwa. Siamini. Nimeumia sana.
 
Kikosi kamili hiki hapa
Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona)
Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Emre Can (Liverpool), Jonas Hector (Cologne), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shkodran Mustafi (Valencia), Antonio Rudiger (Roma)
Viungo: Julian Draxler (Wolfsburg), Mario Gotze (Bayern Munich), Sami Khedira (Juventus), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Schalke), Bastian Schweinsteiger (Manchester United), Julian Weigl (Borussia Dortmund)
Washambuliaji: Mario Gomez (Besiktas), Thomas Muller (Bayern Munich), Lukas Podolski (Galatasaray), Andre Schurrle (Wolfsburg)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video