Msafara wa Yanga umeondoka alfajiri ya leo saa 12 kuelekea Angola, Siku ya Jumatano (18, Mei) Yanga itawakabili GD Sagrada Esperanca mchezo wa marudiano kombe la shirikisho! Benedicto Tinocco, Said Juma, Issoufou Boubacar na Malimi Busungu wamebaki nchini hawajaambatana na timu.
"Mchezo wa soka una maajabu yake, tunachukua tahadhari hiyo, tunajua lolote laweza kutokea lakini tutawakabili na kuhakikisha tunaingia hatua ya 8 bora (makundi) kombe la shirikisho barani Afrika"Alisema Hans Pluijm dakika chache kabla ya msafara huo kuiacha ardhi ya Tanzania.
Yanga watashuka dimbani wakiwa tayari na hazina ya ushindi wa magoli 2 - 0 walioupata nyumbani kupitia magoli ya Saimon Anthony na Saimon Msuva.
0 comments:
Post a Comment