Wachezaji wa Yanga wakisikiliza mawaidha ya kutoka kwa makocha wao Hans Van der Pluijm na Juma Mwambusi baada ya kumaliza mazoezi ya mwisho leo na kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Grupo Desportivo Sagrada Esperança, mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa katika dimba la Estádio Sagrada Esperança Dundo huko nchini Angola.
Ushindi, sare ya aina yoyote ama kutofungwa zaidi ya goli moja, kunaihakikishia Yanga nafasi ya kufuzu moja kwa moja kuelekea hatua ya makundi ya Michuano ya Shirikisho na kuzoa mabilioni ya CAF.
0 comments:
Post a Comment