Ni ukweli usiopingika kwamba Manchester United ndiyo klabu kubwa na maarufu kuliko zote za England, wana mashabiki kutoka pande zote za dunia hii, ambao huwa wanaenda Old Trafford kuangalia michezo mbalimbali.
Moja ya mashabiki hao ni Moses, ambaye alisafiri kutoka Sierra Leone kwenda nchini England kuangalia mchezo kati ya United na Bournemouth ambao ulikuwa unahitimisha kinyang'anyiro cha EPL msimu wa 2015/16.
Lakini kitendo cha mchezo huo kusogezwa mbele kutokana na tetesi za kuwepo kwa kiashiria cha mlipuko uwanjani hapo, maana yake ni kwamba, Moses ameshindwa kutimiza azma yake jana.
Lakini hata hivyo, shukrani za pekee ziwaendee mashabiki wa Manchester United kwa ukarimu wao baada ya kujitolea kumsaidia na kumpeleka kunako dimba la Wembley ambapo mchezo huo unataraji kufanyika kesho.
0 comments:
Post a Comment