Manchester City wamefanikiwa kuilinda nafasi yao ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Swansea mwishoni mwa juma. Matokeo hayo yana maana kwamba matajiri hao wa jiji la Manchester watacheza mechi za mtoano (play-off) kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi.
Inatazamiwa kuwa wapinzani ambao wanatajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kukumbana nao katika hatua hiyo ni wabishi kutoka Ujerumani Borussia Monchengladbach au AS Roma ya Italia.
Ikumbukwe kwamba Manchester City katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, walikuwa pamoja na Borussia Monchengladbach wakati AS Roma walipamana msimu uliopita.
Katika mechi za walizokutana na Monchengladbach, City walifanikiwa kushinda mechi zote mbili, huku dhidi ya AS Roma wakishinda moja na nyingine kutoka sare.
Timu nyigine zenye uwezekano mkubwa wa kukutana na City ni pamoja Monaco ya Ufaransa, Anderlecht ya nchini Ubegiji, Fenerbahce ya Uturuki, Sparta Prague na Steaua Bucharest ya Romania.
Ikumbukwe tu msimu ujao Manchester City itakuwa chini ya Pep Guardiola, ambaye kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kufundisha soka anacheza katika hatua kama hiyo.
Guardiola ambaye anasifikia kwa falsafa yake ya soka la pasi nyingi, anatarajiwa kufanya mapinduzi makubwa klabuni hapo ikiwa ni pamoja na kuifikisha timu hiyo mbali zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, baada ya mwaka huu kuvunja mwiko kwa kufika hatua ya nusu fainali ambayo tangu timu hiyo ianzishwe haijawahi kufika.
0 comments:
Post a Comment