Kwa mara nyingine tena kocha wa zamani wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amekanusha taarifa za kujiunga na Manchester United kwa ajili ya msimu ujao.
Mourinho amekuwa nje ya soka tangu mwezi desemba mwaka jana, baada ya kufukuzwa Chelsea kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho kwenye ligi, lakini amesema kwamba yupo njiani kurudi kundini isipokuwa klabu bado ni siri yake.
Mourinho amekuwa akihusishwa vilivyo na kujiunga na United, huku mustakabali wa Louis van Gaal ukiwa bado kwenye kizungumkuti wakati pia kukiwa na tetesi Mreno huyo kuwa kwenye mazungumzo na PSG ya Ufaransa.
Hata hivyo, Mourinho bado amesisitiza kuwa hajafanya mazungumzo na klabu yoyote ile.
"Sijafanya mazungumzo na klabu yoyote ile", Mourinho aliiambia Sky Sports wakati alipoulizwa kama kuna uwezekano wowote wa kujiunga na Manchester United.
0 comments:
Post a Comment