Saturday, May 28, 2016

Kutoka kuwa local derby mpaka vita kubwa ya makocha wawili, pambano la aina yake lililojaa visasi. Hilo si pambano jingine bali ni la fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid litakalopigwa leo kunako dimba la San Siro jijini Milan.
Real Madrid wanaingia uwanjani wakiwania taji la 11 wakati Atletico wao wanafanya hivyo kuwania taji lao la kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Real Madrid wameweka kambani mabao 110 msimu huu na kuruhusu mabao 24 wakati Atletico wameweza kuweka kambani mabao 63 na kuruhusu mabao 18 tu.
Unapoziangalia hizi timu mbili basi utagundua Real Madrid ni timu inayoundwa na mastaa walionunuliwa kwa gharama kubwa sana wakati Atletico ni timu inayoundwa na wachezaji wa gharama za kawaida lakini wenye ari kubwa. 
Vyovyote vile utakavyoungalia mpambano huu, kwanza tambua hili ni pambano linaloashiria kilele cha Champions League, hivyo linabebwa na hisia nzito na linagonga vichwa vya habari vingi duniani. Kwa kuzingatia hayo haya ndio mambo muhimu ya kuangalia

Future ya Zidane bado haieleweki.
Kuiongoza timu mpaka fainali ya Ligi ya Mabingwa huku ukiwa na miezi mitano tu tangu uanze kuwa kocha si kitu cha kitoto, na ukiangalia kwa umakini utaona kwamba Zidane ameifanya Madrid kumaliza ya pili katika msimamo wa La Liga huku ikishinda michezo yao ya mwisho 12 mfululizo, ukijumlisha ule wa magoli 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona. Lakini licha kufanya yote hayo bado Zidane hajaweza kupata uhakika wa kuendelea kubaki kama kocha wa Madrid.
Cristiano Ronaldo anaonekana kuwa na furaha katika msimu huu, amefunga tena magoli zaidi ya 50 kwa miaka 6 mfululizo na kukazia heshima yake kama mfungaji wa muda wote katika klabu ya Real Madrid.
Ronaldo pia amefanya vizuri katika Champions League baada ya kufunga magoli 16 katika michezo 11, akibakisha goli moja tu kuirudia rekodi yake ya kuwa mfungaji aliyefunga magoli mengi kwa msimu mmoja aliyeiweka kwa miaka miwili iliyopita. Mwaka 2014 Ronaldo alifunga magoli 17 kwa msimu mmoja.
Licha ya kuwa kwenye kiwango bora, lakini Ronaldo amepata wakati mgumu sana kuwafunga Atletico kwenye michezo ya hivi karibuni. Katika michezo mitano ya mwisho hajafunga hata goli moja.
Ronaldo pia kwenye hati hati ya kuwa kwenye ubora wake, amekuwa na ufiti wa chini100% tangu alipopata maumivu ya misuli ya paja (hamstring injury) dhidi ya Villareal mwezi April, na kuongeza hofu kwa mashabiki baada ya kuumia tena wakati wa mazoezi Jumanne wiki hii japokuwa taarifa za awali zinasema kwamba yuko fiti kwa asilimia 100 katika mchezo wa leo.
Bahati nzuri kwa upande wa  Real, Karim Benzema na Gareth Bale wanaonekana kuwa fiti kwa asilimia zote japokuwa Benzema anakabiliwa na matatizo kadhaa ya nje uwanja ambayo hata hivyo hayawezi kumwekea kikwazo kwenye mchezo huo.
Bale amefanya vyema msimu huu, akiwa amefuga magoli 19 –licha ya kukosa baadhi ya michezo kutokana na kukabiliwa na majeraha. Kwa ujumla katika mchezo huu wa leo yuko fiti kwa asilimia mia moja.
Staa huyo wa Wales amefunga magoli manne katika michezo sita ya mwisho,  yakiwemo magoli ya dakika za majeruhi dhidhi ya  Rayo Vallecano na Real Sociedad.

Atletico wanataka kulipiza kisasi na kuweka heshima.
Atletico wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na lengo la kulipiza kisasi kutokana na kile ambacho kiliwatokea mwaka 2014, Madrid walisawazisha dakika za nyongeza baada ya Ramos kufunga goli maridadi kwa kichwa. Baadaye Real walishinda kwa mabao 4-1. Hivyo leo watakuwa wakiangalia kuweka heshima kwa kuchukua kombe vile vile kulipiza kisasi.
Atletico pia walishwahi kupata machungu kama hayo mwaka 1974 dhidi ya Bayern Munich. Hans-Georg Schwarzenbeck aliisawazishia Bayern Munich goli katika dakika za lala salama baada ya kuwa nyuma kwa goli 1, goli la Atletico kwa wakati huo lilifungwa na  Luis Aragones. Baadaye Bayern Munich walishinda kwa penati 4-0.
Kombe hili la Ligi ya Mabingwa ndiyo pekee ambalo Atletico wameshindwa kuchukua chini ya utawala wa Diego Simeone, ambaye amewapa  Europa League na Uefa Super Cup mwaka 2012, Copa del Rey mwaka 2013 na La Liga and the Spanish Super Cup mwaka 2014.
Atletico ya Simeone ime-enjoy sana matokeo mazuri dhidi ya mahasimu wao Real kwa miaka ya hivi karibuni wakipoteza mchezo  mmoja tu kati ya michezo kumi waliyocheza tangu ule wa fainali ya Champions League mwaka 2014.
Kufuatia kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kiungo wa zamani wa  Chelsea  Tiago, Atletico wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kikosi kilichokamilika (isipokuwa beki  Jesus Gamez ambaye hata hivyo huwa hatumiki sana), wachezaji wote wako katika ubora wote.

Uwepo wa Fernando Torres ni suala la kuchungwa.
Kama leo unawauliza mashabiki wa Atletico Madrid kama wangependa nani aanze mbele ya safu yao ya ushambuliaji basi moja kwa moja watakwambia ni Ferndando Torres ambaye amekuwa na bahati sana kwenye michuano hiyo tangu akiwa Chelsea.
Torres amefunga mabao sita katika michezo kumi ya mwisho, likiwemo goli muhimu la robo fainali ya UEFA dhidi ya Barcelona huku akiwa na maelewano mazuri na mshambuliaji mwenza Antoine Griezmann, ambaye pasi iliyotokwa kwa Torres aliitendea hali dhidi ya Bayern baada ya kufunga goli mujarab lililowapeleka moja kwa moja fainali.

Torres anaweza kuandika historia nyingine leo baada ya kutwaa kombe hili akiwa na Chelsea mwaka 2012.
Mtu mwingine muhimu katika mchezo wa leo kwa upande wa Atletico   Griezmann, mchezaji huyu raia wa Ufaransa ambaye anamudu kuchezo nafasi zaidi ya moja uwanjani amekuwa na umuhimu mkubwa katika kikosi cha Simeone.
Wikiendi iliyoisha, Atletico wakiwa mazoezini walichezesha kikosi cha akiba na kile kinachotarajiwa kucheza na Real Madrid, ambapo walitumia mfumo wa 4-3-3 ambao unategemewa kutumiwa pia katika mchezo wa leo.
Kitu cha kufurahisha ni kwamba, mchezo uliisha kwa matokeo ya bila kufungana . na hali hiyo inatoa taswira ya kwamba  Atletico ni timu yenye safu ya ulinzi bora isiyo na kifani , kwa maana wanashindwa kufungana hata wenyewe kwa wenyewe.
Vijana hawa wa Simeone wameweza kupata  clean sheets  35 msimu huu, wakiifikia rekodi ya clean sheet ya muda wote La Liga baada ya kuruhusu mabao  18 ndani ya michezo 38.
Kuna wanaume wawili ambao wanampa Someone kiburi cha kutoruhusu bao kwenye safu yake ya  ulizni, hao si wengine bali ni beki mkongwe na kisiki Diego Godin akisaidiana na Jose Maria Gimenez.
Umakini uliotukuka wa safu ya ulinzi ya Atletico umekuwa ni silaha kubwa kwao dhidi ya Real. Wamefanikiwa kupata clean sheets nne katika michezo saba waliyokutana hivi karibuni.
Lakini takwimu hii ya safu bora ya ulizni isikupambaze na kudhani Atletico ni wazuru tu kwenye kulinda, bali wako vizuri katika idara zote, safu ya ushambuliaji ikiwa na wakali kama Griezmann na  Torres, mbavu ya kulia kukiwa na Juanfran na kushoto Filipe Luis, bila ya kusahau ubora wa viungo kama mahiri Saul Niguez na Koke. Kwa ujumla Atletico wamekamilika.
Ni ukweli usiopingika kwamba Atletico hawawezi kufikia ujuzi na ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa Real ambayo imesheheni nyota wanaolipwa fedha nyingi mno , lakini kwa umoja wao uliojaa ari, Real watapata wakati mgumu sana. Lakini yote kwa yote ni je, Real inayotegemea uwezo wa nyota mmoja mmoja utaweza kuiangamiza Atletico ambayo inategemea inategemea nguvu kazi ya kikosi kizima ambacho kimejaa ari na hamasa? Saa 3:45 usiku swali hilo litajibiwa.

Real Madrid vs Atletico Madrid – Takwimu muhimu
  • Real Madrid wamefika fainali ya  Champions League/European Cup mara  14th, hii ni zaidi ya klabu yoyote Ulaya.Kati ka fainali zote hizo, wameshinda michezo 
  • Hii ni mara ya tatu ndani ya miaka mine,fainali ya Champions League imekuwa ikizikutanisha timu kutoka taifa moja (Ujerumani mwaka 2013, Uhispania mwaka 2014 na mwaka huu wa 2016).
  • Ukijumlisha na mwaka huu wa 2016, Madrid kwa sasa wanafikisha fainali 17 za Champions League/European Cup  (14 kwa Real, tatu kwa Atletico), zaidi ya mji wowote Ulaya  (Milan mara 16).
  • Atletico wameshinda michezo saba kati ya 16 ya mwisho dhidi ya Real Madrid katika michuano yote (droo tano, wamepoteza minne).
  • Michezo saba ya mwisho kukutana kati ya Real na Atletico imezaa mabao manne tu (kila mchezo magoli 2).
  • Huu ni msimu wa tatu mfululizo ambapo makocha wamekuwa wakizifikisha timu fainali wakiwa katika msimu wao wa kwanza kama katika michuano hiyo (Diego Simeone 2014, Luis Enrique 2015, Zinedine Zidane 2016).
  • Atletico wamepata 'clean sheets' 15 katika michezo yao 21 ya mwisho, ukijumlisha nne kati ya sita zilizopatikana katika hatua ya mtoano  msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video