Thursday, May 26, 2016

Mshambuliaji mkongwe wa Simba Musa Hassan Mgosi kupitia Simba news amesema kuna vitu viwili ambavyo hatavisahau baada ya msimu huu wa VPL kumalizika huku klabu yake ikiangukia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

“Kuna mambo mengi ambayo yametokea kwenye msimu wa 2015-16 lakini kwa upande wangu, kuna vitu viwili ambavyo siwezi kuvisahau”, amesema Mgosi ambaye hakupata nafasi ya kutosha kucheza msimu huu kwenye kikosi cha Simba.

“Kitu cha kwanza ni mechi kati yetu ya nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Coastal Union. Coastal Union haikuwa timu ya kututoa sisi lakini kwenye mpira hakuna udogo wa ukubwa wa timu inategemea na maandalizi ya timu, iliniuma sana kutolewa na timu kama Coastal”.

“Kitu kingine kilikuwa ni kufungwa mechi zetu zote mbili na watani wetu wa jadi Yanga, katika uwepo wangu Simba muda wote, hatujawahi kufungwa na Yanga mara mbili mfululizo kwenye msimu mmoja, niliumia sana”.

“Naamini chozi langu litakuja kuwarudia wa kwa namna nyingine kwasababu niliumia sana hata sasahivi bado naendelea kuumia kwasababu haijawahi kutokea kwenye maisha yangu nikiwa Simba”.

Mgosi alifunga goli lake pekee kwenye msimu huu kwenye mchezo wa mwisho wa kufunga ligi wakati Simba ilipopoteza mchezo wake kwa magoli 2-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa taifa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video