Tuesday, May 31, 2016

KIUNGO wa wa zamani wa Azam aliyecheza Simba kwa mkopo, Brian Majwega, amemtuhumu kocha wake Jackson Mayanja kwa kumfanyia roho mbaya na kummaliza kisoka.
Majwega ambaye msimu huu hakucheza kwa mafanikio ndani ya Simba, alitoa kauli hiyo juzi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, akidai sababu kubwa ya kudorora kwake ni Mayanja.
Aliandika: “Tunapitia mengi katika maisha, siwezi kumsahau wala kumsamehe mchezaji wa zamani wa kimataifa na kocha, Mayanja kwa alichonifanyia katika maisha yangu. Namshukuru sana kwa kunimaliza kisoka na kuongea ‘utumbo’ juu yangu na kunipakazia mambo, sijui familia yangu imemkosea nini, hata hivyo maisha yanaendelea. Namshukuru kwa funzo alilonipa.”
Majwega alishindwa kupata nafasi kutokana na ushindani wa namba alioupata kutoka kwa kiungo Peter Mwalyanzi ambaye alionekana kupewa nafasi zaidi na kocha wao ambaye naye ni Mganda, Mayanja.
Kutokana na ushindani huo, Majwega aliamua kujiondoa kwenye kikosi hicho na kulalamika kuwa alichotarajia ndani ya timu hiyo kimekuwa tofauti.
Credit:Bingwa

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video