Kwa kawaida kila ifikapo mwisho wa msimu, kila klabu inafanya tathmini kwa wachezaji wao. Baadhi ya timu kama kama vile Liverpool na Manchester United, zimeshaandaa sherehe kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wao bora wa msimu huu kwenye kila idara.
Lakini hata hivyo hakuna zawadi yoyote iliyopangwa kutolewa kwa ajili ya wachezaji waliocheza kwenye viwango vibovu kabisa.
Baada ya hali hiyo, hapa tumeangazia wachezaji watano ambao wamecheza katika viwango vya ovyo kabisa msimu huu:
5. Theo Walcott – Arsenal
Si muda mrefu sana, Theo Walcott alisadikika kuwa moja ya wachezaji ambao ni hazina kubwa ya Arsenal katika siku za usoni, lakini kiwango chake msimu huu kimeonyesha kuwa na shaka kama kweli ni hazina ya klabu.
Msimu huu ulikuwa ni fursa nzuri sana kwake kung'ara kutokana na washambuliaji tegemeo wa klabu hiyo Olivier Giroud na Danny Welbeck kutokuwa kwenye kiwango bora. lakini kitu kibaya kwake ameshindwa kabisa kutengeneza nafasi ya kuaminiwa kama mshambuliaji wa kutegemewa.
4.Eden Hazard
Akiwa kama mchezaji ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Hazard alitarajiwa kuiongoza Chelsea kuwania ubingwa kwa mara nyingine tena msimu huu, lakini cha ajabu amefeli kufanya hivyo. Ukiwa umebaki mchezo mmoja tu kabla ya kumaliza msimu, Hazard amefunga magoli manne tu na kutoa pasi nne za magoli katika msimu huu wa ligi.
3. Christian Benteke
Akiwa amenunuliwa kwa ada ya paundi milioni 32.5, Benteke alikuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha anafanya kama alivyofanya Suarez wakati akiwa Liverpool kabla ya kuhamia Barcelona.
Mshambulizi huyo wa Ubelgiji amefeli kabisa kuthibitisha ubora wa thamani yake , hata hivyo, wenzake ambao walinunuliwa kwa bei ya chini kuliko yeye kama Firmino na Origi wamekuwa wakichezeshwa kwenye nafasi yake. Si mtu mwenye furaha tena Liverpool.
2. Wilfried Bony
Alikuwa ni mchezaji muhimu sana wakati akiwa Swansea hasa kwenye msimu wa 2014/15, na kumvutia kocha wa Manchester City anayemaliza muda wake Manuel Pellegrini na kuamua kumleta klabuni hapo kuchukua nafasi ya Edin Dzeko, ambaye alikuwa akielekea kunako klabu ya AS Roma. Lakini kiwango cha Muivory Coast huyo kimekuwa si cha kuridhisha. Aguero, Silva, Sterling na Iheanacho kwa sasa wanacheza mbele yake katika michuano mbalimbali.
1. Memphis Depay
Depay alisemwa kuwa ndiye ambaye angevaa viatu sahihi vya Cristiano Ronaldo lakini badala yake moja kwa moja alivyosajiliwa na United kutoka klabu ya PSV Eindhoven, alianza kushutumiwa kujishughulisha sana na kununua magari ya kifahari na kutoka na wasichana warembo kuliko kufanya kilichomleta.
Pengine hiyo ndiyo sababu ya yeye kutokufanya vizuri na kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo, ambaye pia alikuwa akivaa jezi namba saba klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment