Thursday, May 26, 2016

SIMBA wanajua kuwa wametimiza misimu minne mfululizo bila kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na sasa wameamua kutuliza vichwa vyao na kuanza kupitia mafaili ya makocha ambao wanaweza kukinusuru kikosi hicho na kukirudisha kwenye utawala wa soka la Tanzania.
Katika mwaka mmoja na miezi kadhaa chini ya uongozi wa Rais Evance Aveva, wameweza kuachana na makocha wanne wakidhani ndio tatizo la wao kutokupata mafanikio lakini sasa wameona timuatimua hiyo imewagharimu, ambapo wanataka kufanya uamuzi utakaowanufaisha msimu ujao.
Kwa kulitambua hilo, Wekundu hao wa Msimbazi wameanza kupitia mafaili ya baadhi ya makocha wakati huu ambao Mganda Jackson Mayanja amemaliza kazi yake ya kuiongoza kipindi cha mpito walipoachana na Dylan Kerr.
Makocha ambao Simba waliachana nao kwenye uongozi huu wa Aveva ni Zdravko Logarusic, Patrick Phiri, Goran Kopunovic pamoja na Kerr na sasa wanaanza kupitia mafaili ya baadhi yao ambao wanaona wanao uwezo mkubwa.
Amini usiamini lakini ukweli ni kwamba, Wekundu hao wa Msimbazi wanatajwa kutaka kumchukua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya, Bobby Williamson ambaye ana jina kubwa na wadau wanasema kama kweli wakifanikiwa kumnasa watakuwa wamelamba dume.
Mbali na Williamson, Wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea kupitia mafaili ya makocha wao walioachana nao hasa Goran ambaye hawakumfukuza na badala yake walishindwana kwenye malipo ya mkataba mpya wakaachana kwa amani.
Goran anapewa nafasi kutokana na kwamba aliishi vizuri na wachezaji na alikuwa mmoja wa makocha aliyependwa sana na mashabiki ambapo wengi wanadai kuwa kama angekuwepo mpaka leo huenda Simba wasingenyanyaswa na Yanga kwa kuitwa ‘Wamatopeni’.
Pia uongozi unatambua mchango mkubwa wa kocha wao wa zamani  Milovan Cirkovic, hasa wakikumbuka jinsi alivyowafunga Yanga mabao 5-0 na sasa wanajadiliana kati ya hao watatu ni yupi wanayeweza kummudu.
Kigogo mmoja wa Simba alilipasha BINGWA kuwa kwa sasa wanaumiza vichwa na hawawezi kufanya usajili wowote mpaka watakapoleta kocha mpya ambaye watampa jukumu la kutafuta wachezaji wazuri kwa kushirikiana na kamati ya usajili.
“Ni kweli kwamba kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kupata kocha na hii ni baada ya Mayanja (Jackson) kumaliza kazi yake kama tulivyokubaliana kwamba mpaka msimu utakapomalizika na tayari umemalizika.
“Kwa sasa tumesitisha zoezi la usajili tukihangaikia kwanza kumpata kocha kwani hatuwezi kufanya usajili wenyewe, hilo tutalifanya kwa uangalifu mkubwa kwani hii timuatimua imekuwa ikitugharimu sana,” alisema kigogo huyo.
Akizungumzia kuhusu makocha hao wanaotajwa alikiri kuwa inawezekana mmoja kati yao akawa kocha mkuu wa Simba msimu ujao ila akasisitiza kwamba wataangalia zaidi dau kama watakuwa na uwezo nalo.
“Unajua kuna mtu kama huyo Bobby Williamson anayetajwa huwezi kumleta kwa dau dogo, huyo ni kocha mzito sana, pia kumbuka tuliachana na Goran kwa sababu hiyohiyo ya dau hivyo ngoja tusubiri mpaka mwisho ndiyo itajulikana nini kinaendelea, mashabiki wetu tunawaomba wasiwe na wasiwasi kwani mambo mazuri yanakuja,” alisema.
Credit:Bingwa

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video