Thursday, May 26, 2016

Manchester United na Real Madrid zimeendelea kukimbiza kwenye nyanja ya utajiri miongoni mwa vilabu 32 vikubwa ulimwenguni. Hii ni kwa mujibu wa taasisi inayo-deal na masuala ya ukaguzi ya KPMG.
Kwa pamoja Real Madrid na Manchester United vimefungana kwa kuwa na mkwanja wa juu.
Miamba ya Katalunya Barcelona wanashika nafasi ya tatu, huku miamba ya soka ya Bundesliga Bayern Munich wakishika nafasi ya nne na washika bunduki wa London wakimaliza nafasi ya tano.
Makamu Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa United Ed Woodward atafarijika sana kuona vitabu vya timu yake vianasoma vizuri licha kutofanya vizuri tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson mwaka 2013.
Katika orodha hiyo vilabu vitano kutoka ligi ya England vimeingia kumi bora.
Kwa kiasi kikubwa mchezo wa mpira wa miguu umebadilika namna ya kuutangaza na hata njia za kuutangaza mchezo huo kwa mashabiki zimebadilika. Kinachotokea uwanjani ni tofauti na kinachofanyika nje ya uwanja.
Si Real Madrid wala Manchester United ambazo zimechukua ndoo ya ligi zao ndani ya miaka mitatu iliyopita lakini bado wana ongoza kwa utajiri katika ulimwengu wa soka.
Wana mashabiki wengi duniani kuliko klabu zote ambazo wanashindana nazo kwa karibu na hilo ndilo linalowapa faida licha kuwa kutokuwa na vikombe kwa miaka ya hivi karibuni.

Hapa chini ni jedwali linaloonesha viwango vya utajiri kwa vilabu 32 ulimwenguni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video