Zdravko Logarusic
Kocha wa zamani wa Simba ambaye sasa anaifundisha Inter Club ya Angola, Zdravko Logarusic amewakaribisha Yanga katika ardhi ya Angola, lakini amewaonya kwamba wanapaswa kuwa makini.
Kwa mujibu wa salehjembe, Logarusic amesema kamwe haitakuwa kazi rahisi kwa Yanga kwa kuwa Waangola wanachotaka ni kusonga mbele na Esperanca ni timu ya matajiri.
“Wanachotaka Esperanca ni kusonga mbele, hivyo itakuwa ni kazi ngumu kwa Yanga. Nimesikia wana kikosi kizuri, hakika wanapaswa kupambana kweli.
“Kama mechi ingekuwa inachezwa Luanda, ingakuwa rahisi kwa Yanga. Lakini kwao Esperanca lazima kuwe na ugumu,” alisema.
Tayari Yanga iko nchini Angola tayari kwa maandalizi ya mwsiho ya mechi hiyo ya pilik ya Kombe la Shirikisho.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, bila ya Donald Ngoma na Thabani Kamusoko, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment