Tuesday, May 24, 2016

Muda na wakati wowote kutoka sasa Manchester United watamtangaza Jose Mourinho kama kocha mpya wa timu hiyo.
Watu wengi wanaamini ujio wa Mourinho kwenye klabu ya Manchester United si sahihi kutokana na pande zote kuwa na falsafa zinazotofautiana.
Lakini kikubwa kinachomleta Mourinho United si kingine bali na makombe tu. Hilo ndilo suala ambalo limekuwa liwatesa United kwa kipindi kirefu tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson. Ikumbukukwe kuwa United wamekuwa wakisuasua kiasi cha kukosa matokeo hata kwa timu dhaifu, kitu ambacho huko nyuma hakikuwa kikitokea mara kwa mara.
Ikumbukwe tu United wameshinda kombe la FA, hilo ni jambo jema lakini si kwa kiwango cha kuwasahaulisha mashabiki na machungu wanayopitia kwa sasa. Wamekuwa ni wa kiwango cha kawaida sana kwa miaka takribani miwili iliyopita. Si rahisi hata kidogo kwao kunyanyua mdomo na kupinga ujio wa Jose Mourinho klabuni hapo.
Ni ukweli usiopingika kuwa Mourinho ana mapungufu yake ikiwemo kuingia katika rabsha za hapa na pale na waandishi, makocha wenzake, marefa pamoja na maafisa wa FA. Lakini mbali ya yote hayo yeye ni mtu sahihi wa kuifanya United kurudi katika ubora wao. Huyu ni kocha mwenye njaa ya ushindi wakati wote.
Ana rekodi ya kushinda mataji katika nchi zote nne alizowahi kupita kufundisha soka. Ameshinda ligi ya mabingwa mara mbili - amefanya hivyo akiwa na FC Porto ya Ureno pamoja na Inter Milan tena katika sehemu zote hizo akishinda makombe matatu kwa mpigo (treble).
Achana na uwezo wake wa kuvikusanya vikombe vya ndani kama FA, Capital One na kadhalika, huyu ni mtu mwenye asili ya upambanaji na asiyetaka masihara kwenye kazi kitu ambacho United ndiocho wanakitaka haswa.
United wanamhitaji kwa sababu ya kuwapa mashabiki, washika dau na hata wachezaji imani na kuweza kutemebe kifua mbele mbele ya wapinzani wao kama vile mahasimu wao wakubwa wa jiji la Manchester, Manchester City ambao msimu ujao watakuwa chini ya Pep Guardiola.
Wanamhitaji Mourinho kuhakikisha kuwa hayatokei kama ya Liverpool kwamba kucheza UEFA kwao imekuwa ni kama bahati.
Ujio wa Mourinho United ni pigo kubwa kwa mashabiki wa vilabu vingine. Kamwe wasingependa kumwona akirejea na kutua United kwa sababu wanajua fika United iliyo chini ya Van Gaal ingeendelea kuwa ya kawaida na isiyoleta hofu yoyoye kwa timu pinzani, lakini Mreno huyo ataifanya United iwe ni timu yenye kupigania ubingwa kwenye kila michuano inayoshiriki kama ilivyokuwa katika nyakati za Sir Alex Ferguson.
Ni ukweli usiopingika kwamba staili ya mpira wa Mourinho si ya kuvutia wala kusisimua.
Lakini anajua vizuri namna gani ya kuirudisha timu kwenye mstari pale inapopotea. Kitu kizuri kwake ni kwamba si mtu mwenye kutaka sifa ya kucheza mpira wa kuvutia pale anapoona mpinzani wake amemzidi mbinu bali hutumia mbinu mbadala ili kumdhibiti mpinzani wake.
Akiwa na klabu ya Real Madrid miaka takriban sita iliyopita, mchezo wake wa kwanza dhidi ya Barcelona, alifungwa mabao 5-0. Mwaka mmoja baadaye akawafunga bao 1-0 na kunyanyua ndoo ya Copa Del Rey ambayo ndio ilikuwa ya kwanza akiwa nchini humo (ya kwanza kwa Madridi tangu msimu wa 2007-8).
Ukweli i kwamba hata mashabiki wa timu kama ya Arsenal wangependa kuwa na kocha wa iana yake hasa baada ya kupita miaka mingi bila timu yao kunusa mafanikio.
Mwaka mmoja baadaye akiwa hapo hapo Madrid aliifunga Barca ya Pep akielekea kubeba ndoo ya La Liga. Huo ulikuwa ni ushindi wao wa kwanza kwa mahasimu wao hao wakubwa katika soka la Hispania kwa takriban miaka minne na ushindi wa kwanza katika dimba la Nou Camp kwa miaka mitano.
Alivunja rekodi ya ufungaji kwa klabu kwenye ligi baada ya kuiongoza kufunga magoli 109.
Mourinho ndiye aliyeipa ubingwa wa kwanza Chelsea baada ya miaka 50 wakipata pointi ambazo hawakuwahi kupata tangu kuanzishwa kwa timu hiyo.
Vivyo hivyo kwa upande wa Inter Milan, walikuwa wakipata mfululizo wa matokeo ya kawaida chini ya kocha Roberto Mancini. Mourinho alipochukua timu tu aliipa ubingwa wa UEFA, Serie A na kombe la ligi. Kwa maana nyingine alichukua makombe matatu kwa mpigo (treble)
Tangu alipoondoka Chelsea hawakuwahi tena kunusa ubingwa wa EPL mpaka alivyorudi msimu wa 2013/14 na kuchukua ndoo ya EPL msimu wa 2014/15 na kombe la Capital One. Hii yote inadhihirisha kwamba Mourinho ni mtu sahihi wa kuirudisha United katika ubora wake. 
Na ndiyo maana licha kupata matokeo mabovu msimu huu ulioisha lakini mashabiki wa Chelsea bado walikuwa na imani naye kutokana na kuamini kwamba alikuwa ni mtu sahihi wa kuipeleka mbeke klabu yao
Ni figisu tu za wachezaji ndizo zilizomng'oa Mourinho Chelsea.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video