Monday, May 23, 2016

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litaendelea kuwaweka kitimoto wachezaji wote waliotenda makosa ndani ya msimu huu ambapo mpaka sasa hukumu zao hazijatolewa akiwemo Donald Ngoma na Amissi Tambwe, wote wa Yanga.

Kwa muda mrefu, Ngoma na Tambwe kesi zao zimekuwa zikipigwa danadana na Kamati ya Nidhamu ya TFF ambapo wachezaji hao kila mmoja ana kesi yake ya kimaadili.
Ngoma anatuhumiwa kumpiga kichwa beki, Hassan Kessy wakati Yanga ilipopambana na Simba, huku Tambwe naye akituhumiwa kumshika sehemu za siri Juuko Murshid pia timu hizo zilipokutana.

Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, wanajua kwamba kamati ya maadili ya shirikisho hilo haijamaliza kusikiliza baadhi ya kesi zilizopo mezani kwao zikiwemo za wachezaji hao huku ligi ikiwa imemalizika, hivyo wameahidi kutenda haki kama kuna ambaye atakutwa na hatia ataadhibiwa kwa nafasi yake hata kama ni msimu ujao.

Mwesigwa alitaja sababu za kesi hizo kupigwa danadana nyingi ni kwamba, kamati husika mara kwa mara watendaji wake wamekuwa hawakamiliki kila wanapotakiwa kukaa kujadili na wanapokamilika utakuta wachezaji hao wana majukumu kwenye timu zao.

“Hata kama ligi inaisha kesi zao zipo palepale, haiwezekani ligi iishe halafu kesi nazo ziishe, hapo tutakuwa hatujatenda haki.

“Kamati ya nidhamu itakaa siku yoyote hata kama ligi imeisha na maamuzi yatakayotoka yatatangazwa na kama kuna adhabu basi wahusika watatumikia adhabu zao msimu ujao,” alisema Mwesigwa.
Credit:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video