Leo Manchester United wanavaana na Crystal Palace katika mchezo wa fainali ya kombe la FA utakaopigwa kwenye dimba la Wembley.
United hawakuwa na msimu mzuri baada kuishia hatua ya makundi UEFA na kudondokea michuano ya EUROPA ambayo hata hivyo walitupwa nje na Liverpool, hivyo kombe la FA ni muhimu sana kwao ili kufuta machozi ya machungu waliyopata.
United pia wamekosa nafasi ya kufuzu kucheza UEFA mwakani baada ya kushika nafasi ya tano nyuma ya Leicester, Arsenal, Tottenham na Manchester City.
Hata hivyo wakati United ikiwa chini ya Sir Alex Ferguson, kombe la FA lilikuwa kama ziada tu hasa baada ya kuibuka mabingwa wa ligi kuu, ukizingatia ya kwamba walikuwa wakishinda mara kadhaa kwa pamoja ubingwa wa ligi kuu na makombe mengine likiwemo FA.
Hivyo basi, United wameamua kwamba endapo watashinda ubingwa wa FA leo, kamwe hawatafanya 'bus parade' kwenye jiji la Manchester kwa kuwa si kitu chenye uzito mkubwa kwao.
Bus parade hufanywa na timu zinazochukua makombe mbalimbali ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuwaonyesha mashabiki kombe/makombe waliyochukua.
0 comments:
Post a Comment