Harry Kane na Jamie Vardy jana wameonesha kwamba wao ndio pacha sahihi ya England kwa sasa kuelekea michunao ya EURO 2016 kule nchini Ufaransa baada ya kila mmoja kufunga bao moja katika ushindi wa England wa mabao 2-1 dhidi ya Uturuki.
Lakini kuna utata mkubwa kwenye goli la Kane ambalo linasadikika lilikuwa ni la kuotea (offside).
Kutokana na kukerwa na maamuzi ya mwamuzi kukubali goli hilo, kocha wa Uturuki Fatih Terim aliamua kumfuata mwamuzi namba nne (4th official) na kuamua kumuonesha kwa kutumia simu yake aina ya iPhone namna goli lile lilivyokuwa offside.
Hii ni tukio jipya, mara nyingi makocha huishia kulalamika tu lakini huwa hawafanyi kama alivyofanya kocha wa Uturuki.
Uthibitisho wa video ya kocha wa Uturuki.
0 comments:
Post a Comment