Tuesday, May 24, 2016

Baada ya leo mchana kutoka taarifa kwamba Cristiano Ronaldo ameumia na huenda angeikosa fainali ya Champions League dhidi ya Atletico Madrid wikiendi hii, hatimaye Ronaldo ameongea na waandishi wa habari na kutoa maendeleo ya afya yake.
Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba mashabiki wa Real Madrid hawana haja ya kuwa na wasiwasi baada ya kuondoka mazoezini Jumanne ya leo akiwa ameumia baada ya kugongana na kipa Kiko Casilla.
Madrid walikuwa mazoezini kuelekea katika mchezo wa jumamosi hii katika dimba la San Siro dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid asubuhi ya leo na ndipo Ronaldo alipongana na Casillas na akaonekana kupata maumivu yaliyopelekea kuondoka uwanjani akiwa anachechemea.
 Hata hivyo, mshambuliaji huyo ameongea na waandishi wa habari, na kuwaambia kwamba yupo fiti kwa asilimia 100.
“Nipo sawa. Katika siku chache zijazo nitakuwa fiti kwa asilimia 100.”
Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa kwenye kiwango kizuri sana kwenye mashindano ya ulaya – akifunga magoli 16 katika mechi 11 akiwa anaelekea kuivunja rekodi yake ya magoli 17 aliyoiweka miaka miwili iliyopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video