Tuesday, May 31, 2016

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta anaamini kwamba Real Madrid pia watakuwa na huzuni kutokana na kukosa taji la La Liga licha ya kushinda taji la Champions League kwa mara ya 11.
Cristiano Ronaldo alifunga penati ua ushindi na kuipa timu yake ushindi wa 5-3 dhidi ya Atletioc baada ya dakika 120 kumalizika kwa bao 1-1, fainali iliyopigwa jijini Milan mwishoni mwa wiki.
Hata hivyo, Iniesta amewakejeli Real kwa kukosa ubingwa wa La Liga kwa miaka minne mfululizo.
"Sisi hatusherehekei eti kwa sababu Madrid ameshinda taji la Champions League au la", Iniesta amesema.
"Sisi tunasherehekea ubingwa wetu wenyewe, tuna furaha na mafanikio yetu na kuhuzunishwa na matokeo yetu mabovu kwa upande mwingine.
"Real wamechukua ubingwa wa Champions League lakini vile vile watakuwa wakihuzunishwa kwa kukosa La Liga, hivyo mashabiki wetu, ma sisi kama timu, ni lazima tujivunie msimu mzuri ambao tumekuwa nao."
Iniesta aliongeza: "Bilashaka kufeli kwetu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa ni fedheha kubwa, lakini mwakani nadhani tutapambana kurudi kwenye mstari."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video