Miaka takribani mitatu tangu uhamisho wake wa kwenda Arsenal kufeli mshambuliaji GONZALO HIGUAIN ameandika historia ya ufungaji katika ligi kuu ya Serie A.
Mshambuliaji huyo wa Napoli jana alifunga hat trick na kutimiza magoli 36 katika msimu mmoja wa Serie A – magoli mengi zaidi ya mchezaji yoyote tangu Gino Rossetti alipofunga idadi hiyo akiwa na Torino mwaka 1929.
Pia gwiji wa soka wa Sweden, Gunnar Nordahl alifunga magoli 35 akiwa na Milan mwaka 1950.
Na Sasa Higuain amekuja kufikia na kuivunja rekodi hiyo kwa magoli mazuri katika dimba la San Paolo.
Higuain, 28, alifunga magoli matatu ndani ya dakika 20 katika kipindi cha pili katika mchezo wa ushindi wa 4-0 dhidi ya Frosinone.
Higuain, ambaye ameifikia rekodi hiyo akicheza mechi 35, ni mchezaji wa tisa wa Argentina kushinda kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa Serie A.
“Nilikuwa na matamanio mazito makubwa ya kuivunja hii rekodi na inanibidi kumshukuru kila mmoja, familia yangu, jiji la Napoli, wafanyakazi, klabu, na timu yangu,” alisema Higuain.
0 comments:
Post a Comment