Pep Guardiola ameelezea kipindi chake cha miaka mitatu aliyokaa Bayern Munich kama moja ya nyakati bora katika maisha yake ya soka. Alisema kauli hiyo punde tu baada ya kutwaa ndoo ya 'DFB-Pokal' kutokana na ushindi waliopupata dhidi ya Borussia Dortmund.
Bayern waliibuka na ushindi wapenati 4-3 baada ya dakika tisini za mchezo kuisha bila kufungana. Shujaa wa Bayern alikuwa ni Manuel Neuer baada ya kuokoa kwa umahiri penati za Sven Bender Sokratis.
Kwa ushindi huo, maana yake ni kwamba Guardiola anawaachia Bayern msimu huu makombe mawili kabla ya kuondoka kuelekea Manchester City huku akibubujikwa na machozi baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo na wakati wa kukabidhiwa kombe.
"Nilikuwa na waati mzuri sana hapa", alisema. "Ningependa tu kusema kwamba nawatakia kila la heri katika siku za usoni.
"Nimefarijika kumaliza msimu kwa namna hii - tumetosheka vizuri kabisa. Nitawakumbuka wachezaji wengi sana.
0 comments:
Post a Comment