Kocha wa Hispania Vicente Del Bosque amewaacha mshambulaiji wa Chelsea Diego Costa, kiungo wa Manchester United Juan Mata na kiungo wa Arsenal Santi Cazorla katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 25 kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya EURO mwaka huu yatakayofanyika Ufaransa.
Costa hakuwa na katika kiwango bora msimu huu hasa mwanzoni mwa ligi huku akifanikiwa kufunga mabao 16 tu katika michuano yote msimu huu, hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kutemwa katika kikosi hicho.
Hata hivyo, badala yake Del Bosque ameamua kuwachagua washambuliaji Alvaro Morata, Aritz Aduriz na Nolito kama wachezaji pekee watakaounda safu yake ya ushambuliaji.
Fernando Torres, ambaye amekuwa na msimu mzuri sana katika klabu yake ya Atletico Madrid, pia ameachwa kwenye kikosi hicho.
Hector Bellerin amefanikiwa kuitwa kwa mara ya kwanza kabisa kwenye kikosi hicho, akiungana na mabeki wenzake wa kulia Juanfran na Dani Carvajal wa Real Madrid.
Kikosi kamili hiki hapa;
0 comments:
Post a Comment