BEKI wa Yanga Vicent Bossou anafurahia ubingwa wake wa kwanza akiwa na Yanga lakini amepata taarifa njema baada ya kurejeshwa tena katika kikosi cha taifa lake la Togo.
Kocha mpya Mfaransa Claude LeRoy ndiye aliyefanya maamuzi hayo baada ya kupata taarifa njema za Bossou hasa baada ya kupata mechi alizocheza na klabu yake hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari barua ya mualiko wa kujiunga na timu ya taifa lake imeshafika Yanga katika ofisi ya katibu wao Baraka Deusdedit kwa beki huyo kujiunga na timu hiyo itakayoingia kambini wiki chache zijazo kuumana na Liberia.
“Kweli nimeitwa kujiunga na timu ya taifa, Yanga wameshapokea barua hiyo ya mualiko na kunijulisha, kwangu ni taarifa nzuri kwa kuwa nakwenda kulisaidia taifa langu baada ya kuisaidia klabu yangu kutwaa ubingwa sasa najiunga na taifa langu,” amesema Bossou.
Mara ya mwisho kwa Bossou kuitwa Togo ni wakati kikosi hicho kikicheza na Uganda wakati huo ikifundishwa na kocha Mbelgiji Torm Saintfiet ambaye hata hivyo hakumchezesha hata mara moja.
0 comments:
Post a Comment