Barcelona wamefanikiwa kuchukua kombe la mfalme maarufu kama Copa del Rey baada ya kuwafunga Sevilla mabao 2-0.
Katika mchezo huo uliotawaliwa na ubabe wa aina yake, mabao ya Barcelona yalifungwa na Jordi Alba katika dakika ya 97 baada ya kupata pasi murua kutoka kwa Leo Messi.
Neymar aliifungia Barcelona goli la pili kwenye dakika ya 120 baada ya kupoke pasi nzuri kutoka kwa Messi.
Katika mchezo huo zilitoka kadi nyekundu tatu, moja kwa upande wa Barcelona na mbili kwa uoande wa Sevilla.
Kwa upande wa Barcelona Javier Mascherano alipata kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Kevin Gameiro dakika ya 36, huku Sevilla kwa upande wao Ever Banega alitolewa baada ya kumfanyia faulo Neymar katika dakika ya 90 na Daniel Carrico alitolewa nje pia kwa kumtole lugha chafu mwamuzi baada ya hapo awali kuwa na kadi ya njano aliyoipata kutokana na kumfanyia faulo Leo Messi.
Video ya magoli hii hapa;
0 comments:
Post a Comment