Beki wa kulia wa Atletico Madrid Juan Francisco Torres maarufu kama 'Juanfran' alifunga penati ya ushindi kwenye Champions League hatua ya 16 bora wakati timu hiyo ilipoitoa PSV Eindhoven lakini ni juyo huyo ambaye amekosa penati ya ambayo imewakosesha ubingwa wa UEFA baada ya kufungwa na Real Madrid Jumapili usiku.
Juanfran (31) ambaye ni raia wa Hispania ndiyo mchezaji pekee kwenye mchezo huo aliyekosa penati wakati Real Madrid wakibeba ndoo ya Champions League kwa ushindi wa penati 5-3.
Baada ya mchezo huo wachezaji wa Atletico hasa Juanfran walijawa na huzuni kubwa kiasi cha kuwaomba radhi mashabiki wao kwa kile kilichotokea.
Leo ameamua kuandika barua maalum kwa mashabiki wa Atletico Madrid ambayo pia imeshewa katika ukurasa rasmi wa Instagram wa Atletico de Madrid.
BARUA INASOMEKA HIVI;
Hello Atleticos,
Nimeomba klabu kuwafikishia barua juu ya kila kitu ninachojisikia
Kamwe sitasahau moyo wa dhati mlioonesha kwangu wakati nilipokuja kwenu kuomba msamaha. Nikiona machozi yangu yakitiririka mbele ya maelfu ya mashabiki wa Atletico waliofika uwanjani na kunisaidia kuendana na uhalisia wa huzuni kubwa iliyokuwa imejaa kwenye nafsi yangu. Vile vile bila ya kusahau sapoti niliyopata kutoka kwa wachezaji wenzangu, kocha na watu wote wanaounda familia hii ya Atletico.
Pia ningependa kuwashukuru kwa imani kubwa ambayo mara zote mmekuwa mkionesha kwetu, na zaidi ya yote ni kutufanya kujiona watu wa tofauti wengine na wenye nafsi ya kipeke kutokana nauwepo wetu hapa Atletico.
Miaka miwili iliyopita, niliwaambia kwamba tungerejea tena fainali, na tumefanya hivyo, sasa, nawaambia kwamba, Gabi, nahodha wetu hivi iwe hivi karibuni au baadaye atanyanyua kombe la Champions League na kusherehekea sote kwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment