Wednesday, May 25, 2016

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo walikosea kuvifanya katika msimu huu, ni kutotumia vyema nafasi ya usajili wa wachezaji wa kimataifa.
Simba mpaka sasa ina wachezaji saba wa kigeni ambao ni, Juuko Murshid, Brian Majwega, Hamis Kiiza (wa Uganda), Emery Nimubona (Burundi), Paul Kiongera (Kenya), Justice Majabvi (Zimbabwe) na kipa, Vincent Angban wa Ivory Coast ambao uongozi huo una mpango wa kuachana na wachezaji hao isipokuwa Angban pekee.  
Aveva alisema ubutu wa viwango vya wachezaji hao ndiyo ilikuwa moja ya sababu kwa klabu hiyo kushindwa kutamba kwa msimu huu tofauti na wapinzani wao Yanga ambao walilamba dume katika usajili wao kama wa Donald Ngoma wa Zimbabwe ambaye ameonyesha kiwango cha hali ya juu.
“Kiukweli kwa msimu huu moja ya vitu ambavyo sisi tulichemsha ni kuhusiana na usajili wa wachezaji wa kigeni ambapo tulishindwa kabisa kuzitumia hizi nafasi saba ambazo tulipewa na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kuwasajili wachezaji hao.
“Utaona kuwa sehemu kubwa ya wachezaji hao viwango vyao vilikuwa ni vya chini na havikuwa vikiruhusu kucheza Simba kutokana na wao kushindwa kuwa sehemu ya msaada ndani ya timu.
“Lakini tumepata fundisho kwa msimu huu na tunajipanga kwa msimu ujao kuhakikisha kamati yetu ya usajili inaleta wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ambao wataweza kutusaidia kufanya vizuri,” alisema Aveva wakati akiongea na Salehjembe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video