Mtandao wa 101greatgoals unaripoti kuwa, licha ya kuwa haijathibitishwa rasmi na tovuti ya klabu ya Arsenal, lakini ukweli ni kwamba Arsenal wameshakalimisha usajili wao kwanza kabisa katika dirisha la kubwa la majira ya joto baada ya kumnyakuwa kiungo mkabaji raia wa Uswizi Granit Xhaka, anayekipiga kunako klabu ya Borussia Monchengladbach.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kwamba, makubaliano na kiungo huyo yalimalizika jana usiku na kufanikiwa kufuzu vipimo vya afya vilivyofanyika kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa London Colney jioni hii.
Xhaka ameshafanya mahojiano ya kwanza akiwa kama mchezaji wa Arsenal huku akiwa amevaa uzi wa Arsenal utakaotumika msimu ujao.
Kiungo huyo mzaliwa wa Kosovo, alikuwa akiwindwa vikali kwa muda mrefu na kocha Arsene Wenger na kufanikiwa kumsajili tafsiri yake ni kwamba, ameanza mchakato wa kuziba mapengo ya kina Flamini, Arteta na Rosicky ambao wamemaliza mikataba yao msimu huu.
0 comments:
Post a Comment