Friday, May 27, 2016

Carlo Ancelotti anaelezea hisia zake juu ya mwenendo wa soka hasa katika masuala ya kiutawala wakati alipokuwa kaihojiwa na kituo cha Talksport.
Bosi huyo mpya wa Bayern Munich – ambaye amechukua mikoba ya Pep Guardiola anayeelekea Man City – ameandika kwenye 'autobiography' yake, ambapo ndani yake amezitaja timu za Chelsea, PSG and Real Madrid, timu ambazo aliwahi kufundisha katika nyakati tofauti.
Ancelotti amezungumzia siasa na pesa kama mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa kuumiza mchezo wa soka kwa sasa ulimwenguni akirejea hasa yaliyotokea ndani ya Arsenal na Manchester United.
Anaitaja ligi ya England kama ligi yenye utajiri mkubwa duniani lakini si ligi bora tena kutokana na kuendeshwa kwa kiasi kikubwa kwa fedha, hali ambayo imepelekea kupoteza ubora wa ligi hiyo.
Ameigusa Manchester United moja kwa moja: Katika msimu huu uliomalizika United wamemaliza katika nafasi ya tano, nafasi ambayo si nzuri kwao hata kidogo lakini cha kushangaza wanashikilia rekodi ya kuwa klabu inayoongoza kwa fedha ulimwnguni ikifungana na Real Madrid, fedha hizo zikitokana na mauzo ya bidhaa na mikataba ya udhamini.
Ancelotti anaammini kwamba kupungua kwa ubora wa United na Arsenal ni kutokana na namna ambavyo timu hizo zinaendeshwa kibishara zaidi:
“Kinachotokea kwa klabu za Manchester United na Arsenal ni cha kushangaza.
“Makocha wote wawili, Wenger na Ferguson (kocha wa zamani wa Man United),wamefanya mambo makubwa sana kwa miaka yote waliyodumu klabuni hapo.
“Nadhani tofauti kubwa iliyopo kwa sasa ni kwamba wamiliki wa Arsenal na Manchester wametoka katika vilabu vya Marekani, hawa si watu wa mpira hata kidogo.
“Kuna mambo mawili katika nyanja ya soka – suala la matokeo uwanjani na masuala ya kifedha. Nadhani Arsenal na Manchester United wanaangalia zaidi masuala ya kifedha kuliko matokeo ya uwanja.
“Unaweza kujikuta mwaka mmoja unaweza kuchukua ubingwa wa ligi na kufika pengine fainali ya UEFA lakini wamiliki wa vilabu hivyo hata hawaguswi, wao wanaangalia zaidi fedha. Kwa mfano vilabu kama AC Milan (ya miaka ya nyuma) na Real Madrid, kwao kitu muhimu ni matokeo na si vinginevyo.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video