
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumatatu kati ya Tanzania dhidi ya Chad utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu. Kiingilio hiki ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya Machungwa
Tiketi za mchezo huo zitaanzwa kuuzwa kuanzia kesho Jumapili katika vituo vya Karume, Mbagala, Buguruni na Ubungo.
Viingilio vingine vitakuwa ni elfu ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, na elfu ishirini na tano.
Wakati huo huo, kikosi cha Chad kinatarajiwa kuwasili nchini leo usiku tayari kwa pambano hilo muhimu katika mbio za kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment