
Kikosi cha Taifa Stars kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza leo jioni tangu watue kutoka Chad walipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Chad.
Hata hivyo, wachezaji wawili, mlinzi tegemeo, Kelvin Yondani na kiungo mchezeshaji, Mwinyi Kazimoto hawakufanya mazoezi jioni ya leo yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa.
Yondani alishindwa kutokana na tatizo la misuli kubana. Baada ya pambano la kwanza dhidi ya Chad, Yondani alipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kubanwa misuli.
Kazimoto aliumia dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza. Hata hivyo hali zinaendelea vizuri na wanaweza kuanza mazoezi kesho.
Credit:Soka 360
0 comments:
Post a Comment