Friday, March 25, 2016

KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amesema mchezo wao dhidi ya Al Ahly ya Misri utakuwa mgumu kutokana na ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwabana, kiasi cha kukosa nafasi ya wachezaji wake kupata muda wa kupumzika.

Yanga itacheza na Al Ahly Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 9 mwaka huu, lakini Yanga ikitakiwa kucheza mechi tatu za viporo vya Ligi Kuu ndani ya siku 11, jambo ambalo Pluijm ameliita ni kuwachosha wachezaji wake.

Pluijm alisema ratiba hiyo mpya imevuruga mipango yake ya kuongeza umakini katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly.

“Nilikuwa na programu za mazoezi ambazo nilikuwa nimeziandaa kwa ajili ya mchezo wetu na Al Ahly, lakini kwa ratiba hii ni kama imeharibika kwa sababu mechi za viporo tunazocheza ni ngumu ambazo tulazimika kucheza kwa nguvu ili kupata ushindi, lakini nyingine ni za mikoani hivyo inatubidi kusafiri,” alisema Pluijm.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema, kwa kiasi kikubwa ratiba hiyo haikuzingatia ushiriki wao kwenye michuano ya Afrika na imewapa wakati mgumu kujipanga.

Alisema kutokana na ratiba hiyo wanalazimika kufanya mazoezi mara moja kwa siku ili kuwapa muda wa kutosha wachezaji wao waweze kupumzika, ili kupata nguvu za kupambana kikamilifu katika mechi zijazo.

Katika marekebisho yaliyotangazwa juzi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara yanaonesha kuwa Yanga itaanza mechi zake za viporo Aprili 3 kwa kuikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na siku tatu baadaye itacheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo huo.
Credit:Soka 360

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video