Klabu ya Simba leo asubuhi kupitia msemaji wake Haji Manara imewasilisha barua rasmi ya kutoa malalamiko yake pamoja na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uendeshwaji wa ligi kuu katika ofisi za makao makuu ya TFF na ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Pamoja na suala hilo la kuwasilisha barua, msemaji wa Simba
Haji Manara amethibitisha kuwa Uongozi wa Simba umemwandikia mchezaji wake Abdi Banda barua ya kumtaka kujieleza kwa nini asipewe adhabu za utovu wa nidhamu aliouonesha kwa kocha Jackson Mayanja pamoja na kosa la kugoma kuvaa jezi yenye nembo ya mdhamini.
0 comments:
Post a Comment