Kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger, ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake katika kikosi cha Ujerumani kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich amekuwa akisumbuliwa na majeraha tangu mwanzoni mwa msimu kabla ya kupona na kujitonesha tena mazoezini jana akiwa na wenzake.
Taarifa iliyotolewa juu ya mchezaji huyo inaeleza kwamba, atafanyiwa vipimo vya MRI na baadaye kutibiwa na Dr. Hans-Wilhelm Müller-Wohlfahrt huko jijini Munich.
0 comments:
Post a Comment